Habari zilizotufikia hivi punde zinasema mchezaji huyo wa zamani wa Yanga na kocha wa Pan Africa amefariki dunia usiku huu baada ya kusumbuliwa na saratani ya koo kwa takriban miaka miwili. Hivi majuzi alitolewa hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa zaidi ya majuma mawili. Msiba uko nyumbani kwake Mwananyamala B Kwa Mama Zakaria
Kilambo na vijana wake wa Yanga Kids siku Kassim Manara aliporudi nyumbani
baada ya kukaa ulaya kwa miaka kibao
Marehemu Athumani Kilambo (kanzu ya kijani) enzi za uhai wake akiwa na wakongwe wenzie wa Pan African Saad Mateo (kushoto) na Kitwana Manara (wa pili kulia)na Nyumba Kipikipiki. |
Marehemu Athumani Kilambo (wa pili nyuma kushoto) akiwa na kikosi cha Yanga kilichotembelea Brazil mwaka 1974. Hapa ni uwanja wa Maracana |
baada ya kukaa ulaya kwa miaka kibao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...