Ndege anapokua hai huwa anakula sana funza, lakini anapokufa funza humla yeye......Maisha yanabadilika kila wakati, hivyo basi usimdharau wala kumuumiza mtu yoyote katika maisha haya.
Kwani unaweza ukawa imara sana leo, ila kumbuka maisha ni imara kuliko wewe......na elewa kuwa mti mmoja unaweza ukatengeneza mamilioni ya njiti za kiberiti, lakini muda ukifika njiti moja tu ya kiberiti inaweza ikachoma msitu mzima......
Hivyo kuwa mwema kwa kila mtu.....coz huwezi jua.
Jumapili njema kwa wadau wote!
naona kitu 'PC' hicho cha Biil Gates hapo mezani. Hiyo unawasha saa moja kabla ya kuanza kutumia
ReplyDeleteGood message,got you broda wa Italy.. Vipi Papa alishachaguliwa? We need a black Papa and not otherwise. Luckson Papalla.
ReplyDeleteBaraka wa Chiberiti
ReplyDeleteUmenena vyema sana, pana utamaduni mbaya sana wa sisi kwa sisi kudharauliana na kuwekana chini sana kana kwamba labda wengine wenzetu wana Ubia au Mkataba na Mwenyezi kuhusu hatma zetu za Maisha ya baadaye.
Ni kweli huwezi kujua, hii dunia unapita tu ni vile uneyemdharau leo kesho utakuja kuona aibu ukikitana naye akiwa juu!