Ndege anapokua hai huwa anakula sana funza, lakini anapokufa funza humla yeye......Maisha yanabadilika kila wakati, hivyo basi usimdharau wala kumuumiza mtu yoyote katika maisha haya. 

Kwani unaweza ukawa imara sana leo, ila kumbuka maisha ni imara kuliko wewe......na elewa kuwa mti mmoja unaweza ukatengeneza mamilioni ya njiti za kiberiti, lakini muda ukifika njiti moja tu ya kiberiti inaweza ikachoma msitu mzima......

Hivyo kuwa mwema kwa kila mtu.....coz huwezi jua.

 Jumapili njema kwa wadau wote!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. naona kitu 'PC' hicho cha Biil Gates hapo mezani. Hiyo unawasha saa moja kabla ya kuanza kutumia

    ReplyDelete
  2. Good message,got you broda wa Italy.. Vipi Papa alishachaguliwa? We need a black Papa and not otherwise. Luckson Papalla.

    ReplyDelete
  3. Baraka wa Chiberiti

    Umenena vyema sana, pana utamaduni mbaya sana wa sisi kwa sisi kudharauliana na kuwekana chini sana kana kwamba labda wengine wenzetu wana Ubia au Mkataba na Mwenyezi kuhusu hatma zetu za Maisha ya baadaye.

    Ni kweli huwezi kujua, hii dunia unapita tu ni vile uneyemdharau leo kesho utakuja kuona aibu ukikitana naye akiwa juu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...