Na Abdulaziz,Lindi
Hospital ya mkoa wa Lindi(Sokoine hospital) imenusurika kuungua usiku wa kuamkia leo kutokana na kilichotajwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Muuguzi wa Zamu ,Bi Rehema Mbinga alieleza kuwa Moto huo ulioanzia katika swichi ya Umeme uliweza kudhibitiwa vyema kufuatia huduma ya haraka ya kuzima moto iliyokuwepo hospitalini  hapo.
 Hata hivyo alieleza masikitiko yake kufuatia simu walizopiga katika kikosi cha kuzima moto cha Manispaa ya Lindi na mpokeaji kujibu majibu rahisi ya Acheni kutania nyie na kukata simu kila ikipigwa.
 "Mwandishi tunashukuru kwa msaada wa wauguzi wenzangu tumefanikiwa kuzima moto huo ulioanzia katika dirisha la kutolea dawa
"Ila fikisha ujumbe Kikosi cha zimamoto waache dharau na majibu rahisi wanapopigiwa simu vinginevyo watasababisha maafa. leo sijui ingekuwaje kama tusingewahi kuuzima huo moto"limalizia Bi Rehema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Duh! Hatari! Bora waliuzima mapema. Kweli ingekuwa hasara kwa wananchi wanaoitegemea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...