Kikosi cha ukaguzi cha makao makuu ya Tanesco kimeendelea na kamata kamata za wezi wa umeme na leo mashine ya kukoboa na kusaga ya Kikuyu Community Development ya mjini Dodoma imebambwa ikitumia nishati hiyo kwa wizi. Hawa wamekutwa wakitumia umeme usiopitia kwenye mita. Mmiliki wa mashine hakuweza kupatikana amedai yupo Dar es Salaam. Anasakwa.
Mashine ya kukoboa na
kusaga ya Kikuyu Community Developmen t ya Dodoma mjini iliyokamatwa kwa wizi
wa umeme
Mita iliyoongez ewa
waya mdogo rangi nyekundu upande wa kulia wa mita
Jengo la mashine ya kukoboa na kusaga ya Kikuyu Community Development,
iliyokamatwa kwa wizi wa umeme
Mnakamata lakini hamtuarifu hizo kesi zinakwishaje?
ReplyDeleteHuu umeshakuwa mchezo wa RUSHWA we unataka kujua iliishiaje? Issue nyingi sana zimesharipotiwa lakini ulishasikia mwisho wake?
ReplyDeleteOfisi zote za Tanesco zina vishoka na wako busy nao humo maofisini mwao, lakini hata siku moja hawakatwi. Umeme huo ni mkubwa na wanaojua mbinu za kuiba ni wao Tanesco na vishoka.
Ukienda issue muhimu za matatizo LUKU, kubambikiwa bili, umeme kukata baadhi ya phase n.k. mtazungushwa mpaka ukome.
Hivi ndivyo nchi yetu Tanzania inavyotafunwa na watu wachache!!!
Wanaujamaa nanyi mnakuwa wezi?
ReplyDelete''KIKUYU COMMUNITY DEVELOPMENT''
Ama kweli pana tofauti kubwa sana kati ya Ujamaa wa Kipindi cha Ujamaa cha Kambarage , Wanaujamaa wa sasa wa zama za Ufisadi na Ubepari!!!
Hawa TANESCO hawana lolote...wanaenda kukamata biashara za walala hoi wakati wanaogopa kwenda kukamata viwanda vya wahindi na wachina wanaoiba umeme mwingi zaidi...sheria za nchi hii ni kali kwa wazawa kuliko wageni..
ReplyDeleteingawa swala hapa ni kuibiwa kwa umeme wa Tanesco, lakini mimi ningependa kujua hii Kikuyu Community Development infanya nini huko katikati ya Tanzania. N kama ni wakukuyu wa Kenya, je makaratasi wanayo ya kufanyia kazi? maana si tu wanaiba an kufanya vitendo kunyume na sheria za service company bila pia wanaiibia nchi kwa ujumla. Na kama hawana makaratasi wanaiba utaifa wa Tanzania pi. Tafadhali wahusika fuatilia hilo. Je wanaiba tu au wanaishi nchini kinyume na sheria. Kama hamtawafuatilia mkatoa jibu nitalifuatilia mimi privately na kuwafungulia mashtaka kama watabainika kuwa wahalifu wa uraia.
ReplyDeleteTANESCO kazi yenu hiyo hiyo, hapo hakuna cho chote bali mmenyimwa mshiko mliozoea kuchukua, matokeo yake hizo gharama za hasara mnatuingizia sisi wanyonge kwenye luku kisha mnasema kuwa tunadaiwa madeni ya nyuma. Hakuna kitu kimenikela kama walichofanya TANESCO mteja anadaiwE deni la mwaka 2000 wakati sheria ya luku ilikuwa kwanza unakamilisha deni ndipo unawekewa luku. Kisha wamekuwa wezi wao kwa kutorudisha fedha za mteja ambae amelipa isivyo halali. Lakini mwisho wenu uko karibu. TANESCO IVUNJWE TUMECHOKA NAYO!!!
ReplyDelete