Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba,Sheria na Utawala Bora Dk.Pindi
Chana (wa tatu kutoka kulia)akizungumza na viongozi wa Ofisi ya
Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakati wa ziara ya kamati yake katika
ofisi hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu Serikalini Bw.Emmanuel
Mlay (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu Mfumo Shirikishi wa Taarifa za
Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Katiba,Sheria na Utawala Bora.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.HAB
Mkwizu (aliyesimama)akiwasilisha kazi za ofisi yake kwa Kamati ya Bunge ya
Katiba,Sheria na Utawala Bora ilipofanya ziara ofisini hapo.
Wajumbe wa Kamati ya Katiba,Sheria na Utawala Bora wakiangalia jinsi Mfumo
Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini
(HCMIS)unavyofanya kazi kupitia mtandao katika ziara waliyoifanya Ofisi ya
Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya Bunge ya Katiba ,Sheria na Utawala Bora
Mh.William Ngeleja (MB)(wa pili kulia) akichangia mada wakati wa ziara ya
kamati hiyo katika Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Mwenyekiti msaidizi utawala bora!!! Ehe Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteKAma ofisi hii imeweza kujenga hall ambalo linatumika kama la mikutano , kusomea a.a. training, kwanini ofisi nyingine za serikali hazifanyi hivi ili kuokoa mapesa ya kupanga mahoteli makubwa makubwa kwa training hizi? Ankal upo karibu na rais tunaona utufikishie malalamiko yetu haya, kila ofisi ya serikali iwe na hall lake kubwa kuaccomodate watu wake kwa ajili ya mikutano na training, posho jamani za nini wakati mtu yupo ofisi hapo hapo? hebu na rais awe mzalendo KODI ZETU ZINATUUMA, NA TUNASALI SANA KUSHITAKI KWA MWENYE EZ MUNGU JUU YA KODI ZETU JAMANI TUNAUMIA SANA
ReplyDeleteNamuona Mr Ntukamazina mbunge wa Ngara,nilikuwa sijamuona muda mrefu sana naona hajabadilika
ReplyDelete