Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Anna Abdallah akizungumza na maofisa
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Kamati hiyo ilifanya ziara ya ukaguzi wa
mipango ya maendeleo ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam jana. Aliyevaa tai ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Pereira Ame Silima.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akizungumza na wajumbe wa
Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama na maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya ukaguzi wa mipango ya maendeleo ya jeshi
hilo, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Anna Abdallah akifurahi jambo wakati
alipokuwa anakagua na kamati yake ujenzi wa makao makuu ya Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji linalojengwa Tazara Mchicha, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kushoto-aliyevaa tai)
akiwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama wakati walipokuwa
wanakagua ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (aliyevaa tai) akiwa na
wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama wakati walipokuwa wanakagua
ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es Salaam.
PICHA
ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...