Na Waandishi wetu-MAELEZO_Dar es Salaam.
 
Kamati ya  Bunge  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano kimataifa imeshauri Serikali kutoa fursa kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi kuja kuwekeza  nchini katika sekta mbalimbali ili kukuza uchumi wetu.
 
Kauli hiyo imetolewa leo na wajumbe wa Kamati hiyo ilipokutana na viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya bajeti ya mwaka 2013/2014
 
Walisema wakati umefikwa kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kutowekewa vikwazo katika kupata taarifa muhimu  zinazohusu sekta mbalimbali za uchumi ili waweze kuja kuwekeza badala ya fedha zao kukaa nazo nje ya Tanzania.
 
Waliongeza kuwa ni vema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikaunda Kitengo maalum cha diplomasia ya uchumi kitakachoshirikisha  wataalamu wa sekta mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utangazaji wa fursa za uwekezaji nchini kwa ili kuboresha nyanja za uchumi kupitia Watanzania waishio nje.
 
Akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Kamati hiyo Naibu Waziri wa Wizara wa Mambo ya Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Maalim alisema kuwa Serikali hivi sasa inaendelea kutangaza fursa mbalimbali ambazo zipo Tanzania ambapo tayari wawekezaji kutoka Oman wameshaonyesha nia ya kuwekeza nchini.
 
Alisema kuwa wawekezaji hao wanakusudia kununua nyama ambapo pia watajenga machinjio ya kisasa ambayo yatatumika kuchinjia mifugo kabla ya nyama haijasafirishwa kwenda nje ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani,nielewesheni,kamati inasema diaspora(watz ughaibuni),majibu ya foreign ministry wanasema Oman ndio wamepewa. Hapo swali/jibu yanawiana vipi?

    ReplyDelete
  2. Uwekezaji nchini:

    Katika hiyohiyo BAJETI na Sekta ya Fedha, ili tupige hatua nchini mambo haya ni muhimu haraka tuyarekebishe:

    Sio kuishia kutoa Fursa kwa Madispora waishio nje kuwekeza nchini bali pia uwekezaji ufunguliwe kwa wananchi walio nchini kuwekeza ktk mambo kama,

    1.Manicipal Bonds,
    2.T-Bonds and T-Bills,
    3.Sovereign Bond ianzishwe haraka,
    4.Portifolio Management,
    5.PE(Private Equity) zinahitajika ziongezeke zaidi.

    Nchi yetu Tanzania ina rasilimali nyingi huku Idadi ya Makampuni yaliyo orodheshwa ktk Masoko ya Hisa DSE hayazizi 20 wakati Kenya yenye Rasilimali chache kuliko sisi ina Makampuni yaliyo orodheshwa (NSE-Listed Companies) yanafikia karibu 100 (mia moja) huku nature ya Asset zao zikiwa ni biashara au Assets za Makampuni ya Majani ya chai na Kilimo cha Mauwa.

    Tumeshaondoka kwenye Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na sasa tupo kwenye Ubepari. mashariti haya cchini inastahili yafutwe:

    (i)Kwa kuwa tunazo Rasilimali nyingi nchini na pia tuna kusudia kupunguza kasi ya Umasikini na kwa kuwapa Fursa za kuwekeza na kushikilia Rasilimali wananchji wa kawaida tuondoe Shariti la Ukomo wa Manunuzi ya hisa ktk Soko la Hisa DSE kuweka kiwango cha Hisa zisizidi 60%. iwe mnunuzi hasa mwananchi anunue kwa uwezo wake atakaoweza.

    (ii)Kuwa ruhusu watu wa kawaida ktk Biashara ya uwekezaji ktk Bonds na Portifolio Management.

    (iii)Company ACT. (Corporate Governance)

    Kuongeza Shariti la Makampuni kujiorodhesha ktk Masoko ya Hisa hasa kampuni zenye Mitaji mikubwa na zile zinazokuwa na Asset za Rasilimali kama Gas, Oil and Mineral Sector.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Kwanza, ''Jamii ya Madiaspora wa Kitanzania'' ipo nchi zote Duniani ambapo wapo watu wenye asili ya Tanzania.

    Oman ni mojawapo katika nchi za Dunia ambayo ina jamii Kongwe sana ya 'Madiaspora wa Kitanzania', hivyo Mhe.Mahadhi alimaanisha Madiaspora wa Tanzania waliopo Oman ndio tayari waliopewa fursa ya Uwekezaji huku Jamii zingine ktk nchi zingine zikitazamiwa kufikiwa na mipango hii pia .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...