Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na ujumbe wake, wakionyweshwa maumbo ya namna kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, wakipata maelezo kwa video, kuhusu kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akitazama kiatu, wakati yeye na msafara wake walipotembelea kiwanda cha viatu cha Huajian mjini Dongguan, China, alipotembelea kiwanda hicho, Machi 13, 2013, akiwa katika ziara ya mafunzo, nchini China. Wengine kutoka kwa Kinana ni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Yusuf Mohamed Yusuf.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. .Mwenye kumbukumbu, nini kilikuwa chanzo cha maneno CHAMA CHA MAPINDUZI(Mapinduzi gani haya yalikuwa?).Nimesoma bango huko ndani linasomeka ".....Revolutionary party"(Chama cha mapinduzi),kwa kiingereza Revoulitionary Party linakuwa zito kidogo,nimejaribu kusoma maana ya Revolutionary Party nikakutana na mambo ya Marxism na Leninism nikaachana nayo(Magumu sana).

    David V

    ReplyDelete
  2. Anony wa kwanza, chama ni itikadi au kwamfano rahisi chama ni kama dini. Dini inakuelekeza sehemu fulani, chama chochote pia kinakuelekeza mahala fulani, kwa hiyo basi inawezekana mtu binafsi akaiona dini fulani ni ngumu na haielewielewi na mtu huyo huyo akatokea kuielewa vema na kuikubali dini nyingine. Dini inayoeleweka kwako ndiyo dini yako maana itakufikisha peponi. Kama huelewi dini yoyote basi kaa bila dini ila tukikuchagua uongozi lazima tukuapishe kwa njia uijuayo wewe. Kwa hiyo basi
    kulinganisha CCM na mambo ya kina Marx na Lennin yatakuwangisha kichwa. Kumbuka tofauti zilizopo:
    1. Ukubwa wa mataifa
    2. Kipindi/ vipindi tafauti
    3. Siasa za wakubwa (nyakati)
    4. jogorafia
    5. Ukoloni
    6. uchumi wa nchi unazojaribu kuzilinganisha.
    7. Elimu/Kiwango cha watu kuelewa na kuendesha mambo wao wenyewe.
    8. Wapinzani wa ndani na nje.
    9.nk
    Harafu hilo neno MAPINDUZI, linaweza kuwa na tafsiri mbalimbali kufuatana na mahitaji ya jamii au mataifa mbalimbali. kwa mfano hata hiki chama cha mapinduzi cha leo sio chama cha mapinduzi cha enzi za Azimio la Arusha. Tunakubaliana? sijui umri wako, maana kujifunza kwa kuona ni vema zaidi kuliko kusimuliwa. Swali lako ni zuri lakini fanya utafiti kwanza.
    Shukrani.


    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...