Mtunzi mashuhuri wa vitabu kutoka kampuni ya Mkuki na Nyota, Mzee Walter Bgoya, akikata utepe pamoja na mtunzi wa kitabu cha ‘Kifo ni Haki Yangu’, Eric James Shigongo (kulia) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam leo.
Mtunzi wa kitabu cha ‘Kifo ni Haki Yangu’, Eric James Shigongo, akiongea na wadau (hawapo pichani) waliofika katika uzinduzi wa kitabu chake katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora jijini Dar.

Afisa wa polisi Patrick Massawe ambaye pia ni mtunzi mashuhuri wa hadithi za magazeti nchini, akisainiwa kitabu na Shigongo wakati wa uzinduzi.

Eric Shigongo akimsainia kitabu mwanaye, Samwel Shigongo.
Eric Shigongo akisaini kitabu kwa ajili ya mwandishi wa Nipashe, Somoe Ng’itu.
Shigongo akiwasainia vitabu baadhi ya wasomaji waliohudhuria uzinduzi huo.

Afisa wa polisi Patrick Massawe na msomaji mwingine wakipitia baadhi ya kurasa za kitabu cha Eric Shigongo aliyesimama kulia.
Shigongo akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa duka la TPH.
MTUNZI mahiri wa vitabu nchini, Eric James Shigongo, leo amezindua rasmi kitabu chake cha ‘KIFO NI HAKI YANGU’ katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House (TPH) lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo, wasomaji 50 wa mwanzo walipata fursa ya kupata zawadi ya kitabu hicho bure kilichosainiwa na mtunzi. Kujipatia nakala ya kitabu hicho na vinginevyo, wasiliana au fika katika vituo tajwa hapo chini:
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)
--
Posted By Blogger to KAMANDA WA MATUKIO at 3/25/2013 08:30:00 PM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...