Wadau wa tasnia ya filamu nchini wamemvulia kofia mlimbwende na mcheza sinema maarufu nchi Wema Sepetu baada ya kumuokoa msanii mwenzake Kajala Masanja asiswekwe gerezani baada ya kumlipia faini ya shilingi milioni 13 iliyohitajika baada ya hukumu iliyokuwa inamkabili Kajala na mumewe Faraji Agustino kwa kupatikana na makosa ya kutakatisha fedha haramu (money laundering). 

 Mbele ya Hakimu Sundi Fimbo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam Kajala alikuwa keshahukumiwa kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5, ama kutoa faini ya shilingi milioni 13.

 Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe kukumbwa na makosa ya kutakatisha fedha haramu. Baada ya hukumu hiyo kutolewa mahakamani hapo, Wema Sepetu alijitolea kulipa faini hiyo ya shilingi milioni 13 na kumuokoa Kajala asitumikie adhabu ya kifungo hicho cha miaka 5 gerezani. 

 “Hata sifahamu kwa nini watu wanamsema vibaya mtu mwenye roho kama hii aliyonayo Wema (Sepetu) ”, alisema Masudi Bitebo, mla vichwa (kinyozi) maarufu anayetamba katika anga za Mwananyamala B kwenye saluni yake ya Bitebo Jnr Hair Designer, ambako ndiko mwanadada Wema Sepetu hutengenezwa nywele zake. 

Mdau mwingine, Mwarami Popati wa Tabata, amesema kwamba Mola atamlipia Wema Sepetu kwa wema wake, pamoja na kujali maslahi yaw engine. “Piga ua lakini Wema (Sepetu) ni bonge la staa hapa Tanzania. “Ustaa ujue unaanzia moyoni. Haya ya nje ni mwili tu. Wasanii wangapi wanaotengeneza fedha nyingi walikuwepo mahakamani leo. Lakini ni wangapi walijitokeza kumuokoa mwenzao?” alisema Popati.

Kwa habari ya kina ya kesi hii mtembelee mwanalibeneke wa habari za mahakamani Happiness Katabazi BOFYA HAPA
Kajala na mumewe kabla ya hukumu kusomwa leo
Mzee Masanja na baadhi ya wasanii wakitahayri baada ya hukumu
Kajala amwaga chozi baada ya hukumu
Wema Sepetu akiondoka  na Kajala baada ya kumlipia faini ya milioni 13
Mratibu wa shughuli za kumuokoa Kajala, Dokta Sheni akiwa na Kajala baada ya kuachiwa huru.
Picha zote na GPL

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. nimemkumbuka Kanumba angekuwepo! RIP stive kanumba!

    ReplyDelete
  2. Rozari ina nguvu ya ajabu haswa ukijua mana yake na jinsi ya kuitumia, Kajala usiache kusali rozari na sio sasa umetoka jela ndo uitupe katengeneze hata ya dhahabu na uipeleke ikabarikiwe isikutoke shingoni. Wema wewe ni mwema Mungu ndo atakulipa usisubiri kulipwa na wanadamu, wewe umetumiwa na Mungu.

    ReplyDelete
  3. WASANII WAANZISHE CHAMA CHA KUSAIDIANA. WAWEKE HELA BENKI KWENYE Matatizo WASAIDIANE. HONGERA WEMA KWA WEMA WAKO. MUNGU AKUONGEZEE INSHALLAH

    ReplyDelete
  4. HUYU RAY MANENO MENGI TU AKUNA CHOCHOTE ANA CHO KISAIDIA MBONA AMESHINDWA KUCHANGIA KIDOGO KWA MWENZIWE ALIPO ACHIWA LULU ALIJIGAMBA KUWA AMEMSAIDIA MATENDO SIYO MANENO TU YA KUTAKA SIFA

    ReplyDelete
  5. Hilo ni funzo kwa wengine kwamba usicheze na serikali na mahakama.

    Asijione star akadhania yuko juu ya sheria. Sheria ni msumeno binti Masanja.

    ReplyDelete
  6. kuna yatima wanalala njaa kila siku bila kosa wao milioni ngapi?

    ReplyDelete
  7. haha mdau hapo juu una imani kali sana eti rozari imemsaidia

    aliemsaidia ni wema sepetu au rozari?

    nenda kachinje mtu alafu vaa rozari ukiwa mahakamani kama utaachiwa huru

    keep it up with your imani lakini usizidishe mpaka ukamsingizia mungu mambo ambayo sio ya kweli.

    pole sana kajala muombe wema akufundishe mafundisho ya imani ya kiislam hiyo ndio imani ya kweli.

    ReplyDelete
  8. mau malikaMarch 26, 2013

    safi sana nimfano wa kuigwa kwa wasanii wengine. big up wema. mau malika

    ReplyDelete
  9. Tumsifu pia na Cheni amekuwa mstari wa mbele sana kusaidia wenzake hawa kina JB, Richie, Ray, Wolper, Irene Uwoya na wengine wako wapi mbona hawaonekanagi kwenye vitu kama hvi?

    ReplyDelete
  10. Dr. Cheni?!, movie zimeisha sasa uko kitu live

    ReplyDelete
  11. hahaha huyo naye ndo hajui mungu kamuonyeshea wema kajala sali sana rozari na umuombe sana mungu wako na uishi vizuri na watu rozari ndio mpango mzima..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...