Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kulia kwake) aliyeongozana na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Serikali ya Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mark Simmonds (kushoto kwake) aliyeongozana na ujumbe wake wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 22, 2013 kwa amazungumzo. Picha na OMR
======= ====== ======
MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA WAZIRI WA UINGEREZA ANAYESHUGHULIKIA MASUALA YA AFRIKA
DAR ES SALAAM, MACHI 22, 2013
Mheshimiwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal leo Ijumaa, amekutana na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia
masuala ya Afrika Bwana Mark Simmonds ofisini kwake Ikulu jijini Dar es
Salaam ambapo sambamba na masuala mengine akaelezea shukrani zake kwa
serikali ya Uingereza kwa kuwa na mahusiano mazuri na Tanzania na kwa
kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais aliyekuwa anamuwakilisha Rais katika mapokezi hayo
alisema, Tanzania inathamini mchango wa Uingereza katika sekta za elimu
na afya na sasa ambapo kampuni za Uingereza hasa British Gas
inajihusisha katika utafutaji wa Gesi katika bahari ya kina kirefu
Kusini mwa Tanzania. Pia alizungumzia kuhusu mchango wa Uingereza
kimataifa hasa katika masuala ya Mazingira na akamueleza Waziri Simmonds
kuwa, Uingereza inaweza kusaidia nchi zinazokabiliwa na athari za
mabadiliko ya tabia nchi kwa yenyewe kushirikiana na nchi kubwa duniani
katika kuhakikisha kuwa zinatimiza wajibu wao katika kulinda mazingira.
Kwa
upende wake Waziri Simmonds yeye alimshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais
kwa mapokezi mazuri na kisha akaelezea furaha yake kwa mchango wa
Tanzania katika kusaka amani katika nchi za Maziwa Makuu hasa DRC,
Madagasca na Zimbabwe na kisha akafafanua kuwa, Tanzania ni mshirika
mzuri wa Uingereza na kwamba nchi hii ni mfano wa kuigwa kutokana na
ushiriki wake katika kusaidia amani kwa majirani zake sambamba na hatua
zake za kuwapatia maendeleo wananchi wake.
Waziri
huyo alibainisha kuwa Uingereza iko tayari kuendelea kusaidia katika
suala zima la uwazi na uwajibikaji na hasa katika maeneo ya Kodi na
akashauri juu ya kuzidi kuwa na mashirikiano baina ya serikali na sekta
binafsi katika shughuli za maendeleo.
Waziri
Simmonds anakaa nchini kwa siku mbili na katika mkutano huu na
Mheshimiwa Makamu wa Rais alifuatana na Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania Diana Melrose.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam, Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...