Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Kulia ni Mke wa Mzee Kingunge
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika kumjulia hali nyumbani kwake Victoria jijini Dar es Salaam jana Machi 23, 2013 baada ya mzee Kingunge kulazwa Hospitali ya Muhimbili kwa uangalizi hivi karibuni alipougua ghafla. Picha na OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. mimi haya mambo siyaelewi sasa nani mgonjwa hapa mzee kingunge au huyu makamu wa rais ikiwa mzee kingunge ndio mgonjwa kwa nini yeye hakukaa kwenye kochi laini ili apate nafuu badala yake amakaa yule mzima na mgonjwa amekatlia lile la afadhali au ndio protocol basi hata katika maradhi basi ukubwa uwe una mipaka jamani umri na hali ya mgonjwa izingatiwe msipende ukubwa mkasahau utu na heshima.
    ugua pole mzee wetu na akija kiranja mwingine kukutizama muweke chini kama hataki na aende.
    mdau.
    shanghai,peoples republic of china.

    ReplyDelete
  2. Nikuelimishe amekalia kiti kinachomfaa kwa kunyoosha mgongo na ndicho maridgawa kwa mgonjwa. Makochi magodoro laini ni sumu kwa wagonjwa haswa wazee na wenye matatizo ya mifupa na maishipa.

    ReplyDelete
  3. acha ushamba wewe. kuna viti maalum kwaajili ya watu wenye matatizo ya mgongo ambavyo ninakua havibonyei. ndomana umamwona mzee wetu hapo kakalia hicho kiti. Sofa linabonyea na kusababisha mtu kujikunja sehemu ya mgongo wakati mgongo unatakiwa unyooke

    ReplyDelete
  4. hapana mimi nadhani daktari ameshauri akae kwenye kiti hicho vinginevyo kisingekuwepo hapo kutokana na hadhhi ya viti hivyo vingine unavyodai ni vizuri sio kila kizuri ni kizuri kwa afya

    ReplyDelete
  5. Sema KITI cha mzee wetu kama kilikuwa Store muda mrefu,Naona kama Vumbi hivi au macho yangu, Kama ni vumbi basi wafanye utaratibu wa kukifuta na kukipiga ile vanishi sijui tena. Otherwise UGUA POLE BABA YETU and GET WELL SOON.

    ReplyDelete
  6. hata mimi nimeona kiti kinavumbi balaaa..si unaona bongo heee usafi nje sio ndani bonge la aibu aiseee..
    mdau
    ulaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...