Msajili
wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi, (CRB),Eng.Boniface Muhegi (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki kuhusiana na kufutiwa usajili wa wakandarsi 1110 nchini. kushoto ni
Mwenyekiti wa bodi ya CRB, Eng. Consolata Ngimbwa na Msajili Msaidizi
Ukaguzi wa bodi hiyo, Flora Mwombeki (kulia).
Na Ripota Wetu , Dar es Salaam
Bodi
ya Usajili wa Makandarasi (CRB) imesisitiza kuwa wakandarsi 1110
waliofutiwa usajili hivi karibuni waharuhusiwi kufanya kazi yoyote hapa
nchini kwa vile kuendelea kufanya kazi hivyo kutapelekea adhabu kali
zaidi za kisheria.
Msajili
wa Bodi hiyo, Eng. Boniface Muhegi aliwaambia waandishi wa habari
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa wale wote waliofutiwa
usajili hivi karibuni wanatakiwa kurudisha vyeti vya usajili wao kwenye
bodi ya makandarasi kwa sababu kubaki navyo na kuendelea kufanya kazi ni
kinyume na sheria.
Akitoa
sababu za kufutiwa kwa usajili kampuni hizo alisema kampuni 10
zimefutiwa sababu majina yao yalitumiwa na kampuni nyingine zisizo na
sifa; na kampuni 34 kwa kushindwa kutimiza masharti ya usajili katika
mamlaka husika.
Alisema kampuni mbili zilishindwa kusimamia vizuri kazi; tano ziliomba zenyewe zifutwe na kampuni 1059 zilishindwa kulipa ada ya usajili kwa muda unaotakiwa.
Hatua hii ya kufuta usajili wa idadi hii ya makandarasi imepata baraka za kibali toka kwa waziri wa ujenzi, Dkt. John Magufuli.
Alieleza
kuwa kwa kampuni 1059 zilizoshindwa kulipa ada zao kwa wakati, wanaweza
kulipa ada hiyo na faini ili bodi iweze kuangalia taratibu za
kuwarudishia tena usajili wao.
“Kwa
mujibu wa sheria mkandarasi aliyefutiwa usajili haruhusiwi kufanya kazi
tena…hata kama alikua na kazi anaendelea nayo,” alisema, na kufafanua
kuwa waajiri waliokuwa na wakandarasi waliofutiwa usajili wanatakiwa
kutafuta wengine kwani wenye sifa zinazotakiwa wako wengi nchini.
Alisema
mkandarasi aliyefutiwa usajili na kugundulika anafanya kazi atakabiliwa
na kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya asilimia 10 ya mradi wote
anaoutekeleza.
Alisema
bodi kupitia ofisi zake za kanda itaendelea kuwafutia usajili
wakandarasi nchini ambao wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Alitoa
wito kwa wanaotoa kazi kwa wakandarasi kushirikiana vyema na bodi hiyo
kuhakikisha kuwa taratibu zinafuatwa na mafanikio yanapatikana katika
sekta ya ujenzi nchini.
Alisema
kuanzia mwaka 2000, kampuni za kizalendo zimekuwa zikiimarika na
kufanya vizuri na kwamba bodi itaendelea kuzipatia mafunzo na uwezeshaji
wa aina mbalimbali katika kiziimarisha na kuzijengea uwezo.
Alisema
waajiri wote wanaotumia kazi za wakandarasi nchini wanahitajika kupata
ushauri kutoka bodi hiyo ili kupata wakandarasi bora na kupata huduma
iliyo bora na salama.
Hapo bodi husika inatakiwa kubadilisha vyeti na kutoa vipya kwa wale waliotimiza viwango na wenye kutumia vya zamani wajulikane wamezama kwenye utapeli kuliko kuwaomba vyeti warudishe,wabaki navyo kama kumbukumbu abavyo havifanyi kazi,bank kuu zkibadilisha noti zina toa deadline na usiporushisha inakuwa urembo tena,ni mawazo yangu tu.Mdau wenu wa gropu ya jamii
ReplyDelete