MKE wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda amewataka akinamama wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali kuwa waaminifu kwa wenza wao na wanafamilia wao ili waweze kupata ushirikiano kutoka kwao.

Alisema mbali ya majukumu mengi yanayowakabili, akinamama wanapaswa kuwa karibu na familia zao kwani ndiyo msingi mkuu wa Taifa. “Hatuna budi kutoa malezi mema kwa wenza wetu na watoto wetu. Tunapofanikiwa katika shughuli zetu, tusiache kuwa waaminifu kwa wana-familia wetu (akinababa na watoto wetu); tuwaheshimu na kuwaenzi kwa kuwashirikisha kazi tunazofanya ili tuweze kupata ushirikiano wao na baraka zao,” alisema.

Mama Pinda ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumamosi, Machi 10, 2013) wakati akizungumza na wanawake wajasiriamali walioshiriki Maonyesho Maalum ya Batik (Batik Gala Night) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwenye ukumbi wa Hellenic Club, Upanga jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...