Katika mwendelezo wa kukuza Diplomasia ya Uchumi na kupanua wigo wa Utalii wa Tanzania, Ubalozi wa Tanzania nchini Canada ulishiriki Maonyesho ya Utalii ya Outdoor Adventure yaliyofanyika mjini Ottawa tarehe 16&17 Machi, 2013. Maonyesho hayo yalikuwa na mafanikio makubwa kwa kuitangaza Tanzania na vivutio vyake hususan Mlima Kilimanjaro. Wanaoonekana kwenye picha ni Mhe. Balozi Alex Massinda (Katikati), kutoka kulia ni Bw. Richard Masalu, Afisa Ubalozi Ottawa, anayefuata ni Bw. Paul Makelele, Afisa wa Ubalozi, anayefuata baada ya Mhe. Balozi kushoto ni Bw. Rashid Adam wa Kampuni ya Zara Tours iliyoko Toronto na wa mwisho ni Bw. Julio Sanchez wa Zara Tours.
Bw. Richard Masalu akitoa maelezo kwa mmoja wa wageni waliotembelea Banda la Ubalozi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Haitoshi..... sema hivi...TANZANIA LAND OF MOUNT KILIMANJARO...the word mount should be there...!

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha kuwa sisi wakazi wa Ottawa hatuna taarifa ya maonyesho haya. Kwanini msitumie hii blog kutangaza maonyesho?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...