Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bwana Epraim Mafuru anasikitika kuwatangazia kifo cha Mama yake Mzazi Bi. Anastazia Nyate Mugaya Mafuru. 
Ibada na mazishi ni leo Jumapili (3/03/2013) kuanzia saa sita mchana hapa nyumbani Boko na baadae makaburini Bahari Beach jijini Dar es salaam. 
Mungu ampokee mama yetu. Ufunuo 14.13

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Rip mom! Mungu amekupenda zaidi

    ReplyDelete
  2. Ndg yangu Ephraim MAFURU.

    Moyo wangu umeugua sana baada ya kupata taarifa hizi za huzuni kwa kufiwa na mama yetu mpendwa.

    Mama alitupenda sote na alikua kisima kirefu kilicho jaa HEKIMA nyingi na hakika UPENDO wake wa MAMA ulitutosheleza wanawe na jamii yote. Ukweli Kaka MAFURU MUNGU(S.A.W) amempenda zaidi.

    Familia yangu, Wana CCM UK na mimi pia tunakuombea amani hasa wakati huu wa majonzi kwako na familia yako.

    Njia aliyopita MAMA ni ya amani na utulivu. Hakika tutamwona tena siku Bwana atakapo HITIMISHA kadhia ya malimwengu haya.

    Bwana amemtwaa mtumishi wake.

    MAINA ANG'IELA OWINO
    UK

    ReplyDelete

  3. Pole sana bro.

    Janeth Mselemu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...