Mwenyekiti wa Chademan,Mbunge wa Hai na  Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe akiongea na wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Tarime na madiwani.Picha na Habari na CHADEMA
---
Baada ya kikao cha ndani kati ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya ya Tarime na madiwani, kubaini udhaifu wa kiuongozi ulioruhusu kuzuka kwa makundi yaliyokuwa yakidhoofisha utendaji kazi na uhai wa chama wilayani hapa, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amevunja uongozi wa wilaya hiyo (kwa maana ya Kamati ya Utendaji).

Uamuzi huo uliofanyika jana mchana, ulipokelewa kwa mikono miwili na wajumbe wa kikao hicho.

Baada ya kikao hicho cha Kamati ya Utendaji na madiwani wa CHADEMA Wilaya ya Tarime, Mwenyekiti Mbowe alikutana na wanachama na wadau wa chama wa Tarime, kwenye kikao cha ndani, ambapo kwa kauli moja waliupokea kwa furaha uamuzi huo wa kuvunjwa kwa uongozi huo, huku wakiomba nafasi hizo za uongozi zijazwe mapema kwa ajili ya kuendelea kukiimarisha chama.

Uongozi wa chama katika ngazi za kata hadi misingi utaendelea kufanya kazi kama kawaida.

Kwa hatua hiyo, uchaguzi wa kupata uongozi wa Kamati ya Utendaji ya muda, utafanyika ndani ya mwezi mmoja ukisimamiwa na ngazi ya juu

Mwenyekiti Mbowe amewataka watu wa Tarime kutopoteza ari yao ya dhati katika kukisimamia na kukipigania CHADEMA katika kuendesha mapambano ya ukombozi wa pili wa nchi, ambayo ilikuwa ni mfano wa kuigwa wa wanaChadema nchi nzima, kiasi cha watu kusalimiana..."mambo...kama Tarime..."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ndio ninyi Chadema mnataka mpewe Serikali mtutawale?

    Ninyi wenyewe mapanga mikononi hasa huko Mara, kwanza hata kwa uongozi wa kawaida hmtatufaa kwa kuwa hamna sifa za utulivu.

    Wezi wa ng'ombe ninyi, Wawindaji haramu ninyi,Ujambazi ninyi!

    ReplyDelete
  2. Vuguru Mara haziishi kwa kuwa ndugu zetu ninyi wengi wenu ni Wafuasi wazuri wa MARLEY!

    Kwani hatufahamu?, pana jamaa mmoja mtu wa Dar alikwenda ukweni Mara, ile amefika amekaribishwa Ukweni Babu anaandaa misokoto kadhaa na Pepsi wakiwa wamekaa kwa maongezi na kusalimiana, ile anapewa Kiberiti jamaa akasema situmii, ohhh Ukweni walishangaa sana kupata Mkwe Aliyeokoka akiwa hatumii Gongo wala Bangi!

    ReplyDelete
  3. Mhe.Mbowe ,

    Pongezi sana kwa uamuzi huo!

    Jambo kingine kwa watu wa Mkoa huo ungekuwa unafanya uteuzi au kwenda huko kuonana na wana Chdm ukiambatana na Mganga wa Afya ya akili!

    Jamaa hao bangi na gongo nyingi sana na hawasomeki kabisa!

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa Mbowe ndivyo inavyotakiwa, nafasi za uongozi za Cha dema sio za majaribio, ingia ukiwa umeshaamua kutekeleza sera za chama, yaani kumkomboa mtanzania mnyonge na sio vinginevyo. Kujitafutia umaarufu waende kwa magamba.

    ReplyDelete
  5. brother michuzi mbona zefulana inaonekana kuvaliwa na chadema?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...