Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya Katibu Mkuu,  kuhusu maendeleo ya  maandalizi ya Ujenzi wa  Majengo ya Kimataifa  Tawi la  Arusha yatakayotumika kushughulikia umalizaji wa mashauri ya Masalia ya  iliyokuwa  Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR) pamoja na utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu za mahakama hiyo.  
Majengo hayo yatajengwa katika eneo la Laki Laki Jijini Arusha, ujenzi wake unagharamiwa na Umoja wa Mataifa ambapo makadirio yanaonyesha  yatagharimu dola za Kimarekani 8.79  milioni.  Tayari dola za kimarekani 3 milioni za kuanzia  zimekwisha kutengwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.  
Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Tano, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na  Bajeti ya UN, Bw.  Johannes Huisman ameishuruku Tanzania kwa kutoa eneo hilo la Laki Laki.Akizungumza baada ya kuwasilisha wa  taarifa hiyo, Balozi Manongi alisisitiza kwamba  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejizatiti katika kutoa ushirikiano na kuunga mkono kazi ya  utekelezaji wa mradi huo muhimu ili uweze kukamilika kwa wakati. Na kusisitiza kwamba  jambo  la muhimu ni kwa pande hizo mbili yaani  Tanzania na Umoja wa Mataifa kuhakikisha kwamba zinashirikiana  na kuwasiliana kwa karibu katika kila hatua ya utekelezaji wa mradi huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...