Mbunge na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mhe James Mbatia ni mmoja wa mashujaa wasioimbwa (Unsung Heroes) waliofanya makubwa wakati wa zoezi la uokoaji katika jengo lililopromoka leo katika mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam. 
Baada ya kutoka kuaga mwili wa Mbunge wa Chama Cha Wananchi (CUF) Jimbo la Chambani, Salim Hemed Khamis, katika ukumbi wa Karimjee, sio tu alijumuika na wabunge wenzie katika kusaidia kuwatoa katika kifusi watu waliofunikwa baada ya jengo hilo kuporomoka. 
Akiwa mtaalamu wa kushughulikia dharura (Crisis Management expert), Mhe Mbatia alisimama kidete kuhakikisha kuwa shughuli za uokoaji zinakwenda inavyotakikana baada ya kukakamaa na kuamuru askari polisi na walinzi wengine kuondoa umati wa watu uliotapakaa sehemu ya tukio ili kutoa nafasi kwa wahusika kufanya kazi yao kwa ufanisi.
 Globu ya Jamii ilimshuhudia Mhe Mbatia akihaha huku na kule kuweka mambo sawa, na hata kutumia kipaza sauti kuamuru wasiohusika waondolewe eneo la tukio ili kupisha waokoaji wafanye kazi yao. 
Laiti kama asingekuwepo na kuchukua hatua hiyo kazi ingekuwa ngumu maradufu. Mhe Mbatia, bila kujali vurugu na vumbi lililokuwa likitimka, alitumia muda mrefu kuelekeza nini kifanyike, ikiwa ni pamoja na kuamuru uzio uliozunguka msikiti wa Shia Ithnaasheri uliokuwa jirani na jumba lililopromoka kuvunjwa na kupisha vikosi vya uokoaji viwajibike bila shida. Kwa kifupi kuwepo kwake kulifanikisha kazi iliyokuwepo.
Globu ya Jamii inatoa pongezi na shukrani kwa Mhe James Mbatia kwa ushujaa wa hali ya juu aliouonesha, pamoja na wabunge wote waliojitokeza kushirikiana bega kwa began na waokoaji katika dhahma hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mhe James Mbatia
 Mhe James Mbatia akitoa maelekezo kwa Bw Zully Dewji ya nini kifanyike ili kufanikisha kazi
 Mhe James Mbatia, Kamanda Kova na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik
 Mhe James Mbatia akitoa maelekezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hongera sana mheshimiwa James Mbatia! Umeonyesha mfano mzuri wa kuigwa! Viongozi wetu wengi wanapenda publicity kuliko kufanya kazi; walishafika eneo la tukio mapema na hakuna cha maana walichikifanya... wengine nafikiri walivaa gloves na masks kama mapambo....

    ReplyDelete
  2. wataalamu wa polisi/jeshio wako wapi kwenye uokoaji hadi mbatia awe ndio anaongoza??

    ReplyDelete
  3. Hongera mheshimiwa Mbatia
    Malaika

    ReplyDelete
  4. Jembe hilo kati majembe ambayo Tanzania tunayo kwa wakati huu.Nimemuona mara zote akisimama penye ukweli na uhalisia wa mambo bila kuvutwa na hisia au itikadi.keep it up Mh Mbatia!!!!

    ReplyDelete
  5. Namkubali

    ReplyDelete
  6. Pongezi kwa Mbatia. Ila usiishie hapo,jikite katika kuzuia majanga kama haya,,una platform nzuri ya kufanya kazi hii..tuiambie serikali isimamishe ujenzi wa magorofa yote dar es salaam uhakiki mathubuti ufanyike..yasiyokidhi viwango yabomolewe kabla hatujaendelea kupoteza uhai wa wanadamu wengne..hata pengine uhai wa viongozi kama nyie siku ya kuweka jiwe la msingi au ufunguzi mkakumbwa na kuporomoka kwa jengo kama hayo

    ReplyDelete
  7. Sishangai Mhandisi kuwa na mentality hiyo. Big up brother

    ReplyDelete
  8. Hongera jembe mbatia nakukubari,sasa tunasubiri wauza sura ktk TV,waanze kukosoa na kulaumu

    ReplyDelete
  9. EZRA MBISEMarch 30, 2013

    Kiukweli mheshimiwa amekua mfano kwenye jamii yetu nampa pongezi nyingi.Pia mwenyenzi Mungu alaze roho za marehemu mahali pema peponi.AMINA

    ReplyDelete
  10. Kuanzishwe kitengo cha maafa ili kiwe tayari hali kama hizi zikitokea. Kukuza personality cult hakutasaidia maafa mengine yakitokea kwa sababu Mbatia ni mtu mmoja hawezi kufanya kazi vizuri kama hakuna kitengo maalumu.

    ReplyDelete
  11. Ahsante Mheshimiwa Mbatia kila unalolifanya linadhihirisha uzalendo.Be blessed

    ReplyDelete
  12. Sie tunasubiri tu wataalamu wa kuandamana waitishe. Tutaanza Mbeya, kisha Arusha na tutamalizia na Mwanza. Uokoaji ni kazi ya polisi na jeshi kama mdau hapo juu alivyosema. Poleni Taifa na hususan mliopoteza ndugu wa karibu.

    ReplyDelete
  13. Alichokifanya Mh Mbatia kinadhihirisha kwamba tuna haja ya kuwa ama na serikali ya mseto na mawaziri wasio wabunge.Kuendelea kunganinia vyama kunarudisha nyuma maendeleo maana kuna watu wana utalaamu lakini siasa inawanyima uhuru wa kutumia.Sasa tulijua kwamba Mh Mbatia ni mtaalamu wa dharura?
    Pili,suala la maghoraofa ni zuri sana mijini,ni juzi tu tumeona katika blog hii picha ya maghorofa murua hapo Kariakoo,laiki nina mashaka sana na kiwango cha maghorofa yaliyopo nchini mwetu.Licha ya kuwa chukulia hatua hawa wakandarasi na wengineo,lakini kuwepo na udhibiti wa hali ya juu linapokuja suala la ujenzi kuliko ambavyo kwa sasa kila aliyewahi kujenga hata kibanda ni injinia.Lakini pia,sheria iwekwe wazi,mtu anapofanya uzembe unaopelekea vifo vya namna hii,aonekane kwamba ana wajibu kwa professional negligence na kama vifo vimetokea ashitakiwa kwa jinai ikibidi kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia(manslaughter)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...