
Millen Magese akikabidhi hundi ya milioni kumi na tano kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Mhe. Wilman Ndile; kulia ni Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hasnain Murji
Millen Magese akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa mkuu wa wilaya Mtwara kabla ya kuanza ziara ya kutembelea mashuleni.
Millen Magese akiongea kabla ya kukabidhi mchango wake wa milioni kumi na tano kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa na madawati.
Millen magese akiongea na wanafunzi na walimu wakati wa ziara yake mashuleni.





watoto wanashangaa :) makubwa haya.
ReplyDeleteDon't tell me those little girls want to be like her when they grow up.
ReplyDeleteWatu kama hawa hata ukiwachukia, chuki yako Mungu anakurudishia mwenyewe na utalaanika wewe na yeye ataendelea.
ReplyDeleteHuu ni mfano mzuri sana wa kuigwa na siyo ule wa wale viongozi wanafiki wakiwa katika uongozi wanasababisha maafa kwa raia na mara tu wakiacha uongozi eti wanaanzisha charity kama alivyofanya Bill Clinton.
Namuomba Mola amzidishie uhai huyu dada na amlinde na kila baya na wabaya
Anon wa kwanza na wapili.
ReplyDeleteShame on you, sijui ni chuki au you are too judgemental
Hata kama hao watoto watawish kua kama yeye kuna tatizo gani. Wakiwa kama yeye kwa moyo alionao wahat do you think,ni mabadiliko kiasi gani watafanya katika jamii haya nenda wewe ambae ni mfano mzuri wa kuigwa katoe milioni kumi na tano.
Ifike wakati tuwe na tabia ya kusupport mazuri sio kukatishana tamaa. Unafikiri angetaka kuja na hizo hela akaspend nani angemuuliza?Wangapi wanarudi wanaendesha magari y kifahari na kuparty mwanzo-mwisho na wanalipwa hata zaidi ya huyu dada. Kuweni na utu na ustaarabu watanzania huyu dada anastahili pongezi though simjui but ni mfano wa kuigwa na both wanaume na wanawake wa kitanzania.
Actually bure mnamshambulia mtu alietoa maoni yake. Ujio aliouendea huko mtwara ndio watoto wameacha midomo wazi kwanza kavaa kafa ulaya kichwani, mtwara watu ni maskini kwani akienda kiafrika ingekuwaje, acheni ujinga wa kumtetea. Wamarekani wanaleta wafanyakazi kutoka kwao kuja kusoma utamaduni wa watanzania hapa nchini wanaitwa peacecorps, na kitu muhimu ambacho wanaelekezwa kutokifanya ni kuvaa jeans, na viguo vyao vifupi, huwa wanaviacha kabisa na hapa wanashonewa nguo za vitenge na wanavaa vilemba hawavai nywele za kafa ulaya, kwani na wao wanazo hizo nywele kwa wingi. Kila mahali unapokwenda kuna uvaaji wake bwana. Unakwenda vijijini umevaa kama model. Hata akitoka hivyo vijisenti vyake hata ukuta mmoja wa shule haujengi.
ReplyDeleteKutoa Milioni 15 sio mchezo!
ReplyDeleteTatizo kubwa sisi binaadamu tunajishughulisha saaana na mambo ya wenzetu, tena kwa jicho baya kama hao haters hapo juu.
Mtu anamshupalia mwenzake wakati yeye mshupaliaji hata Shs. 1,000 hajatoa, na hana ujasiri huo wa kutoa!
Dada Millen Magese ni Shujaa, tuache dharau na lawama kila kitu ni juu ya Mwenyezi Mungu.