Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Hab  Mkwizu  akifungua Mkutano wa siku mbili kati ya  Bodi ya  Mishahara na Masilahi  katika Utumishi wa Umma na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka utumishi wa umma. Mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili mbinu na mikakati ya kuboresha masilahi na tija kwa watumishi nchini na ulifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi. Tamika Mwakahesya akitoa mada juu ya Muundo na Majukumu ya Bodi hiyo  kwenye mkutano  wa siku mbili wa  wajumbe wa Bodi ya  Mishahara na Masilahi  katika Utumishi wa Umma na Wakuu wa Idara, Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kutoka utumishi wa umma uliofanyika jijini Dares Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu (kushoto) akijadiliana  jambo na wadau wa Bodi ya  Mishahara na Masilahi  katika Utumishi wa Umma wakati wa Mkutano wa Bodi hiyo wa siku mbili uliowahusisha Wakuu wa Idara, Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu kutoka utumishi wa umma uliofanyika hivi karibuni jijini Dares Salaam. Wa kwanza kulia ni Katibu wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Tamika Mwakahesya, wakifuatiwa  na Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Menejimenti ya Rasilimali  watu -Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Lucy Matozi na Mkurungezi wa  Rasimali watu –Bunge, Bibi. Kitolina Kippa 
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB Mkwizu wa tatu kutoka kushoto akiwa  kwenye picha ya pamoja na  wadau wa mkutano wa  siku mbili  Bodi ya  Mishahara na Masilahi  katika Utumushi wa Umma na  wakuu wa Idara, Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu kutoka utumishi wa umma uliofanyika jijini Dares Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bora Maslahi ya watumishi wa Umma yaboreshwe...itasaidia kuinua morali ya kazi na uwajibikaji!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...