Sehemu ya Tatu ya WanaDMV wafanya mjadala wa kushuka kwa kiwango cha Elimu na matokeoa mabaya ya kidato cha Nne wakianza kuelezea Elimu zamani ilivyokuwa na nini kimesababbisha kuporomoka kwa Elimu Je nani alaumiwe na nini kifanyike kuokoa janga hili WASIKILIZE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Nyinyi mliondoka sasa unataka kuchangia nini? Ushauri wenu haufai kwa TZ. Huku TZ mzazi cha kukila hana atashughulika na maendeleo ya mwanae shule?

    ReplyDelete
  2. Ankal, nimesikiliza mjadala mzima, na nimeuona ni mzuri kabisa. Kwa mtazamo wangu kama mwalimu na mdau wa elimu, wamegusia na kufafanua vipengele vyote muhimu. Nawapa hongera, na hongera za pekee kwa Mubelwa Bandio kwa kuandaa na kuendesha mjadala huu.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Kwanza anony wa Fri Mar 15, 02:48:00 am 2013

    Mzazi hana cha kukila, sasa wewe ulitaka apewe chakula na nani?,,,na Serikali wakati nchi ina ardhi kubwa kabisa na Fursa lukuki za kujitafutia uwezekano wa kuyamudu maisha?

    Kama Kilimo utasema hakuna uhakika mvua ni za kubahatisha kuna Ukame je hata Kuuza Genge inashindikana?,

    Kama wewe unasema mambo magumu mbona Wageni kibao wanaoingia nchini kama Wahindi, Mabanyamulenge wanakuja kutajirikia Tanzania hadi wewe mwenyewe tena una-mind na unaanza kulalamika ohhh Wageni wanachuma kwetu!

    Jaribu kuondoa uvivu wa kufikiri!!!

    ReplyDelete
  4. wewe Anonymous # 1 nyie ndo mnalalamika Tanzania haiendelei ni kwa sababu ya watu kama nyinyi.

    Elimu ni ufunguo wa maisha kama hujui uliza utaambiwa au nenda shule uone maisha yako yatakavyobadilika,

    ReplyDelete
  5. Wao mbona hawakukaa kulima wamekimbilia huko Ughaibuni? Utalima na jembe la mkono? Ndio maana watoto wanafeli maana inawabidi wasaidie wazazi wao kulima, kutafuta maji, n.k. Kuna mstaafu wa JWTZ kawekeza pension yake yote kwenye kilimo, uliza alivyokwisha. Pesa yote imepotea hakuna mazao wala ng'ombe. Kafa kihoro. Wahindi kibao wamefilisika huku Bongo, Mzungu wa TTCL kakimbia na deni. Hospitali za binafsi wanafunga kwa hasara.

    ReplyDelete
  6. Mbona zamani watoto walikuwa wanafaulu, kwa hiyo zamani walikuwa hawatembei kwa miguu kwenda shule na walikuwa wanachukuliwa na kurudishwa na school bus? au zamani wazazi hawakuwa na haja ya kutafuta riziki? kinachoongelewa hapa ni kurudisha taaluma kama ilivyokuwa miaka ya zamani hawajasema wanataka taaluma mpya

    ReplyDelete
  7. ushauri wa bure huo, take it or leave it ni kwa manufaa ya maisha ya baadaye ya watoto wenu

    ReplyDelete
  8. Tuache kuwaonea walimu TATIZO NI SERIKALI na tatizo hili lipo kote AFYA,ELIMU,MADINI.....mlolongo unaendelea na kuendelea. Kwa kifupi TUNAVUNA TILICHOPANDA tuache kutafuta wachawi kati yetu, SERIKALI YA PINDA ndio tatizo. Ni wajibu wa serikali kufanya mapinduzi ya sekta zote hasa AFYA na ELIMU, ONGEZA BAJETI, LIPA watendaji na tuache kulipa wabunge na mawaziri ambao sio WATENDAJI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...