Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akimsalimia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum kabla ya Mkurugenzi huyo kuingia ndani ya Kiwanda cha Magereza kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam kukagua maandalizi mbalimbali ya uanzishwaji wa kiwanda hicho. Kulia ni Mdhibiti wa Shirika la Magereza, John Masunga.
Mhandisi wa Mitambo wa Jeshi la Magereza, Shaban Kitolo (kulia) akimuonyesha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum (wa pili kutoka kushoto) eneo ambalo linatarajiwa kutumiwa katika utengenezaji wa kofia ngumu hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi hilo, Kamishna Jenerali John Minja.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna John Minja akimuonyesha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum (aliyevaa nguo nyeusi) maeneo mbalimbali yaliyopo nje ya kiwanda hicho.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum moja ya kofia ngumu zitakazokuwa zinatengenezwa kiwandani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. EU hainunua bidhaa zilizotengenezwa na wafungwa au watoto!!

    ReplyDelete
  2. Nasi tujitahidi ili tununuwe bidhaa zetu , zao watumie wenyewe..EU wanatumia hizo bidhaa zilotengenezwa na watoto , wamepeleka viwanda nchi za Asia na huko ndo imeota mizizi ajira ya watoto

    ReplyDelete
  3. hii helmet inanikumbusha muvi ya anodi shozniga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...