Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Sadifa Hamis Juma akihutubia aktika mkutano wa UVCCM uliofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa shule ya msingi Mkwajuni, Kata ya Kichangani mkoani Morogoro leo Machi 3, 2013, ikiwa ni mwisho wa ziara yake na viongozi wa kitaifa wa Jumuia hiyo mkoani humo, kukagua na kuimarisha uhai wa Chama na UVCCM
Mbunge wa Morogoro, Abdulazizi Mohammed Abood akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM, baada ya kupandishwa jukwaani na Sadifa (wapili kushoto) wakati wa mkutano huo.
 Sadifa akikabidhi kadi ya Umoja wa CCM, kwa mwanachama mpya wakati wa mkutano huo. Jumla ya wanachama 1700 walipewa kadi.
Sadifa na baadhi ya viongozi wakishirikina na wanachama kula kiapo cha CCM baada ya wanachama wapya wa UVCCM kupewa kadi kwenye mkutano huo
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela akihutubia kwenye mkutano huo
 Mmoja wa vijana machachari aliyehama hivi karibuni kutoka Chadema, Mtela Mwampamba akihutubia kwenye mkutano huo.
"Vijana Chadema wanawazingua tu, wanawahamasisha kufanya maandamano ili wawapige picha za kwenda kuonyesha  nchi za nje kwa marafiki  zao kwa ajili ya kupatiwa mamilioni ya fedha", anasema Mwampamba kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya UVCCM Kaka Mpokwa.
VIjana wakiwa wamembeba Mwampamba baada ya kuingiwa na hotuba yake kwenye mkutano huo
Kama Mwampamba, Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Taifa, Juliana Shonza, ambaye amehamia CCM hivi karibuni, akibebwa na vijana wa UVCCM, baada ya 'kuimwagia razi' Chadema jukwaani kwenye mkutano huo.
"Hawa walijaribu kuwapiga mawe ili msifike kwenye mkutano huu, lakini tazama mlivyofurika! Sasa ninasema, Uwezo wa kuwapiga tunao na nia ya kuwapiga tunayo..Tutawapiga, lakini sisi hatutawapiga kwa mawe ila kwa sera zetu makini" akasema Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda wakati akihutubia kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Morogoro, Abdulaziz Mohamed Abood akiongoza msafara wa pikipiki kwenda kwenye mkutano huo
 Vijana wakiserebuka kwa nyimbo za hamasa kwenye mkutano huo
 "Raaaaaaa UVCCM" Vijana hawa wa CCM wakati wa shamrashamra kwenye mkutano huo
Kujimwaya mwaya hakukukoma hadi mwisho wa mkutano. 
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. NAONA CCM NAO WAMEAMUA KUVAA GWANDA MTAIGA KILA KITU LAKINI MSIPOBADILIKA MINDSET ZENU HAITAWASAIDIA.

    HONGERA CHADEMA KWA KUBUNI GWANDA KUMBE LINALIPA.

    MIMISIYO MWANACHAMA WA CHAMA CHOCHOTE ILA NYIE WENYE VYAMA WAOGOPENI WATU VIGEUGEU KAMA HAO WANAOHAMA NA KUANZA KUTUKANA WALIKOTOKA NI SAWA NA MWANAMKE AU MWANAUME ANAPOACHANA NA MPENZI WAKE NA KUANZA KUMKANDIA KWA RAFIKI ZAKE UJUE YEYE NDIYE MWENYE MATATIZO.

    ReplyDelete
  2. Kazi ipo

    David V

    ReplyDelete
  3. it looks like the poor wabongo are rounded to attend these meetings. How on earth can a country have rallies everyday, when are people allowed to go to work? Are these people paid to attne thsed meetings?
    Can someone explain to me please. It makes me sick to see hungry people. CCM and Chadema etc etc please leave these people alone.

    ReplyDelete
  4. With all the technology around, TVs, radios, computers etc etc why all these meetings everyday? How much is the nation as a whole benefing from this crap!!

    ReplyDelete
  5. nchi haina ajira labda, watu wantumia muda wao kwenda kwenye mikutano. Hakuna nchi iliyojengwa kwa mikutano ya hadhara kila siku.

    ReplyDelete
  6. Muhindi/Mwarabu kaona siasa deal kuliko biashara!!

    ReplyDelete
  7. Haroo!!! njaa mbaya sana...na binadamu na akili yake kukosa msimamao ni mbaya zaidi....Ni sawa na mwanamke aneyeolewa hapa, mara pale.... haaminiki huyu.

    Mimi si mshabiki wa chama chochote, ila CCM kaeni chonjo.. msije mkabeba mamruki.

    ReplyDelete
  8. Mbunge kapanda bodaX2 bila kuvaa helmet, hii ni aibu na mfano mbaya kwa wananchi
    Muwaambie hao viongozi watii sheria kama raia wengine

    ReplyDelete
  9. This is a response from M4C.....tit for tat!

    ReplyDelete
  10. kwani akina Slaa wametoka wapi, wamekula CCM wee sasa wantafta vya kwao wenyewe, ala mkuki kwa nguruwe kwa manadamu mchungu, CHADEMA wa nachakachuliwa picha ili watu waonekana wengi katika TV. These CIA tactics hapo 2015 watakapokosa Ikulu wataonesha picha za watu waliowakusanya kule Mbeya. Kumbe ndio hao vijana ambao hawana kazi bila hela hawaendi katika vikao. Na CHADEMA inamiminiwa hela na wafadhili kwelikweli ingawa wanakataa. Hata kupeleka TEAM ya chama nzima mbeya inagharmu pesa nyingi. Hii serikali watakayounda watawatoa wapi watu ikiwa mkutano mmoja wanaenda chadema wote wa dar es salaam.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...