Ankal za leo,
Mie mdau wako wa looongi hapa Helsinki, Finland, ilikozaliwa Blogu ya Jamii mwaka 2005, kama sikosei. Tunashukuru bado unaendeleza libeneke kama umeanza jana vile. Hongera sana!

Mie sina kawaida ya kuomba msaada tutani toka enzi hizo, ila leo limenikaba kooni hivyo nikaona niombe msaada wa haraka nipumue. Maana dah! Nomaaaa!

Ni hivi ankal, mwanangu leo ni hepi besdei ya kuzaliwa kwake, nasi tumealika watoto wenzie kibao kusherehekea. Tatizo ni kwamba watoto hao waalikwa, ambao ni wa mataifa mbalimbali, wote wameweza kuimba wimbo wa "Happy Birthday" kwa kutumia lugha zao, lakini mwanangu kashindwa kuimba kwa Kiswahili ambacho anakifahamu vizuri tu.

Yaani hivi tunavyoongea analia sana baada ya mimi na mama yake kushindwa kumpa maneno ya Kiswahili ya wimbo huo. Nimepiga simu kila kona ya dunia, wapi. Nikaona hebu nijaribu wadau wa Blogu ya Jamii niombe msaada tutani.

Wadau nisaidieni wimbo huo kwa Kiswahili unaimbwaje????
Mdau Helsinki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Ebwanaee duh, birthday zote hizi kila siku lakini hakuna wimbo wakiswahili?

    ReplyDelete
  2. mmmh mmeshindwa ku translate kwa kiswahili?

    hiyo lugha si unatranslate tu na yeye anafurahia

    haya kwa kiingereza maneno haya kwa google translate yanakupa hayo ya kiswahili.

    happy birthday to you, happy birthday to you, happy Birthday dear baby, happy birthday to you. How old are you now? How old are you now? How old are you now...happy birthday to you.

    KISWAHILI

    furaha ya kuzaliwa kwako, furaha ya kuzaliwa kwako, furaha Kuzaliwa wapenzi kuzaliwa mtoto, na furaha yenu. Umri gani sasa? Umri gani sasa? Umri gani sasa ... furaha ya kuzaliwa kwako.

    haya nimejua leo kusafiri sio kuwa mjanja ni akili ya mtu tu kujua na kutenda au kufikiri.

    gnite

    ReplyDelete
  3. HEPI BESIDEI TU YUUU, HEPI BESIDEI TU YUUU, HEPI BESIDEI DIA FULENDIII, HEPI BESIDEI TU YUUUUU.

    ReplyDelete
  4. Inashangaza sana kuona mbantu anageza mila za ughaibuni kama valentines na thanks giving lakini kuimba wimbo wa siku ya kuzaliwa kwa lugha yake anashindwa.

    ReplyDelete
  5. Pole sana mdau
    But be different
    Hii si tabia ya mbantu,sisi hii kitu "bathday" haituhusu,ila watoto wetu push it down our throat,wataka kukaribisha marafiki, wataka zawadi kutoka kwako na kwa marafiki wao.Mafia hao.

    ReplyDelete
  6. Wdau huyu ndugu ameomba msaada, na siyo kulaumiwa. Nakupongeza mdau kwa kukiri kuwa hujui, jambo ambalo ni gumu mmno miongoni mwetu watanzania. Nimejaribu google translation, lakini kilichotokea nilishindwa kujua kama ni muziki au wimbo. Kwahiyo na mimi naungana na we kuwa sijui na naomba kujuzwa na wataalamu wetu wa Kiswahili.

    ReplyDelete
  7. Hakuna kusherehekea birthday kwa WASWAHILI. Mimi tangu nimezaliwa hakuna hata siku moja niliyesherehekea birthday yangu. Nilipofika Ughaibuni nikaona Wadau wakisherehekea na mimi nikajiingiza. Kuna siku husahau kama birthday yangu imefika. Ndio maana hatuna wimbo. Huku Bongo watu wanaimba kwa kiingereza.

    ReplyDelete
  8. HONGERA MWANANGU WEEE HONGERAAA SIKU YA KUZALIWA KWAKO WEE HONGERAAA, MUNGU AKULINDE MUNGU AKULINDE NA MAJANGA MWANANGU OYEEEEH, NA MAJANGA MWANANGU UWEZE SONGA MBELEE OOOH AYEE. HONGERA MWANANGU, HONGERA KWA MIAKA KADHA NA ELIMU ELA AIYEEE.... in bibi Titi's VOICE
    hahahaha i'm just singing

    Mdau mwenzenu Mama Jana lol

    ReplyDelete
  9. sidhani kama ni lazima nyimbo za kizungu ziwe na tafsiri ya kiswahili.... Pili, Hivi hufahamu kwamba 'birthday' na mambo mengine kama 'velentine', nk si mila za kiafrika? Kama hili hufahamu huku ulaya unafanya nini wewe? Mababu zetu hawakusheherekea 'birthday' na mimi sisheherekei sababu naona hizi sherehe na nyingine lukuki za aina hii ni sherehe zinazoneemesha wafanyabiashara tu. Kama wewe unapenda familia yako siku zote unaweza kuienzi hiyo familia yako... as simple as that! Acha kujilazimishia na utamaduni usio wako

    ReplyDelete
  10. Ushauri:Kwanza mfundishe aimbe huo mwimbo kikwenu Mahenge halafu na sie tutakutafasiria Kiswahili.

    ReplyDelete
  11. tatizo hatuna kumbukubu ya kuzaliwa tunaiga tu unazaliwa tz unkujaulaya unakutana ha sherehe hizi unasema kuwa ulikuwa unafayiwa kwahiyo mtoto anakuuliza wimbo wakiswahili ni upi mweleze

    ReplyDelete
  12. Mtoto huyu anatatizo la kujua kiingereza, kama angekijua vizuri kama anavyo kijua kiswahili angeweza kubuni tafsiri hii kama alivyotafsiri Mdau namba mbili hapo juu.
    Au kama anajua kiingereza vizuri basi anatatizo la ubunifu, yaani hayuko shapu katika kubuni mambo, kwadsababu haikuwa lazima umfundishe,ilikuwa awashangaze nyie wazazi wake kwa kuimba wimbo huu kwa kiswahili, kutokuwa na ubunifu huku kunaweza kuwa kwasababu mtoto huyo ni mdogo sana au akili yake nzito katika kubuni mambo.

    ReplyDelete
  13. Mtungie shairi lililotimia katika vina na mizani kisha umtungie na sauti kama taarabu. Hiyo itakuwa kiswahili zaidi.

    MF:
    Leo siku ya furaha,Kuzaliwa twakumbuka
    hakika unasogea, ukubwa unakufika
    Baraka twakuombea, Mola azidi kuweka
    Siku yako sherekea, kuzaiwa twakumbuka

    ReplyDelete
  14. Poleni sana! Mtaalamu wa lugha hapa! Manaosema google tranlsate mnakosea! Tafsiri inahitaji muktadha! Wote waliotafsiri hapo juu huwezi kuimba kwa toni ya kiizungu!
    Sahihi ni;
    Umezaliwa leo x2
    Umezaliwa leo Jonathan iiiiiiii.
    Umezaliwa leo oooo.
    Una miaka mingapi? x2
    Una miaka mingapi Jonathani?
    Una miaka mingapi?
    Halafu unamalizia na vigele gela "lulu lili lululuuuuuuuuuu" ai ai aiiiii!
    Kwa hiyo wale wadau wasio fani yao wawachie wataalamu na sio kubwabwaja! Ninaweza kukutumia recording yake ukitaka'

    ReplyDelete
  15. Mdau uliyepita big up!! we kweli noma,we ni mtunzi wa ukweli,njoo studio kwangu tufanye recording yake kabisa.!!

    ReplyDelete
  16. Jamani mtu kaomba msaada na nyie mnamkandia. Iwapo nyie hamsherehekei siku za kuzaliwa kwa nini mnataka na wengine wote wasisherehekee? Iwapo kwenu mnatumia vyoo vya shimo hiyo haina maana kuwa usitengeneze choo cha kuvuta. Time inekwenda na dunia inabadilika: zamani watu walikuwa hawajui siku zao za kuzaliwa na /or mila zingine za kigiza zilikuwa zinawazuia.Alafu mnaongelea zamani ni zamani hipi iyo? Mie ninayo picha ya pinhole camera iliyopigwa na masister pale St Joseph Nursery mwaka 1967 wakati nasherehekea birthday yangu. Narudia: 1967 wengi mlikuwa bado kuzaliwa na sasa mnaongelea juu ya zamani.... Pia usiende Rome na msafa wako: mbali ya mila zetu nzuri, tujue kuwa tunakaa kwenye society za watu na ni vizuri kufuata yale yao mazuri...Kalagabaho. Blackmpingo

    ReplyDelete
  17. Mdau wa Hlsinki,

    Pole kwa janga lililokukuta la ''kuudharau mpachao kwa msala upitao'' !

    Linalowasumbua mkifika huko uhamishoni na kupewa Uraia wa dhamana wa Kigeni mnajisahau kabisa na kuutupa Ujonongo wenu na haswa lugha yenu ya thamani ya Kiswahili!

    Hebu angalia nakupa mifano ya Madiaspora wakongwe wawili Duniani ili uone tofauti iliyopo kati yetu sisi na wao.

    1.Wayahudi:
    Wamekuwa ni na Jamii kongwe sana ya watu wao walioishi muda mrefu zaidi duniani na maeneo mbali mbali, lakini sio rahisi uonane na Myahudi asiyeweza lugha ya asili yao ya KIEBRANIA hata kama atakaa karne ngapi nje ni lazima awafundishe kizazi chake uko hata siku akikutana na mtu wa jamii yao hana kigeni cha kukosa, ni kuwa Wayahudi, wanatumia lugha yao Kiebrania (Hebrew) ktk mambo mengi kama Ibada, Utamaduni wao na maisha yao licha ya kuwa na Lugha za maeneo waliyopo.

    2.Waarabu:
    Wapo nchi nyingi sana duniani lakini mwarabu Lugha na Utamaduni wake haachi kamwe, ni lazima atatumia lugha zote lakini KIARABU na Utamaduni wa Mwarabu kwao ni muhimu kwa kila mwenye asili ya Uarabu popote alipo duniani.

    Hivyo, ulistahili kumfunza mwanao licha ya Kiswahili pia ulitakiwa mwanao ajue Kiruguru, Kimakonde na Kizigua ikijumuishwa na Utamuni wa Kabila lako na wa Mtanzania kwa ujumla!!!

    ReplyDelete
  18. Mdau uliyeuliza swali nimevutiwa na creativity yako. Yaani swali umeliuliza kimadaha! Umenifurahisha sana. Ningekuwa mimi ningemwambisha kifinnish au kiingereza maana kwa mila zetu mambo ya hepi basdei si yetu ni ya wazungu hivyo hata wimbo inabidi uimbwe kwa kizungi.

    ReplyDelete
  19. Cha msingi, usifuatishe maneno yakawa kama yalivyo kwenye Kiingereza. Utakwama kabisa. Wengine tumeimba hivi:

    Heri ya kuzaliwa
    Heri ya kuzaliwa
    Heri ya ku-za-li-wa
    Mpendwa wetu [JINA]

    Unaweza hata kuendelea kwa tyuni hiyo hiyo:
    Kata keki tule
    kata keki tule
    kata keki tu-u-le
    Kata keki tule

    Kwa kuangalia mapigo:
    Hap-py birth-day to you (silabi 6 lkn YOU ni ndefu = mapigo mawili > 7)
    Heri ya ku zaliwa (silabi 7)
    Pole huku niliko ni asubuhi saa hizi. Kwa hivyo, hii ni kwa mwaka kesho sasa.

    ReplyDelete
  20. heri ya kuzaliwaaaaa
    heri ya kuzaliwaaaaaa
    heri kwako......!!
    heri ya kuzaliwaaa

    ReplyDelete
  21. Fri Mar 22, 12:00:00 am 2013
    Mdau wa komenti hiyo pole sana, kutosherekea bday ni kutokana na wazazi wanamleaje mtoto.

    kama mimi nilikulia nikisherekea na ndugu zangu mpaka tunakua tunaomba wazazi wasitufanyie party tuliona sasa tuanze kuamua sisi tunasherekeaje hiyo ni tulipokuwa tunaenda umri wa miaka 13. na tulikua ikiwa tunaenda za rafiki wengi pia tunaihsi sasa na kumbu kumbu za picha.

    Usiwe na wasi enjoy kusherekea tu as wengi wanasherekea kiaina tofauri na kwa uamuzi wa kibinafsi na utakacho.

    Cheers!

    ReplyDelete
  22. Hii ni kwa wale rafiki zangu mliomshambulia mtoa mada kuwa siyo utamaduni wetu kusherehekea siku ya kuzaliwa. Natumaini nyote mlipokuwa mtoa maoni yenu mlikuwa mmevaa nguo zenu, kitu ambacho ni kinyume na utamaduni wetu. Mlitakiwa kuvaa magome ya miti au kujifunga vibwebwe vya majani makavu kiunoni. Kwa upande wangu naona ni unafiki kuponda 'valentine's day' au birthday eti siyo utamaduni wetu, wakati mnavaa soksi, chupi, boxer, blazia, skin tight, vest, kaputula, suruali, mashati, magauni, blauzi, undeskirts, kanzu,mabaibui, msuli nk ambavyo mnaelewa kuwa ni kinyume kabisa na utamaduni wetu. Nawaomba rafiki zangu mnieleweshe na kunijuza ni mambo gani utamaduni wetu unayaruhusu kuigwa au kutoigwa kutoka nje ya Afrika?

    ReplyDelete
  23. Ukiacha,wachache waliojibu swali la mhusika, wengi wetu,tumejaribu kutoa ushauri,wengine kuponda, lakini katika yote hayo ni katika kuficha ukweli kwamba na sisi pia hatujui. Badala ya kukiri hilo,tunajifanya wajuaji wa kulaumu na kutoa ushauri usioendana na hitaji la muuliza swali. Jibu swali uliloulizwa,kama hujui kaa kimya au sema hujui. Tujifunze kuelewa maswali tuliyoulizwa kwanza kabla ya kukurupuka kuyajibu!

    Namuunga mkono mdau,huyu, ameelewa swali na ametoa mchango wake!
    Anonymous said...

    Cha msingi, usifuatishe maneno yakawa kama yalivyo kwenye Kiingereza. Utakwama kabisa. Wengine tumeimba hivi:

    Heri ya kuzaliwa
    Heri ya kuzaliwa
    Heri ya ku-za-li-wa
    Mpendwa wetu [JINA]

    Unaweza hata kuendelea kwa tyuni hiyo hiyo:
    Kata keki tule
    kata keki tule
    kata keki tu-u-le
    Kata keki tule

    Kwa kuangalia mapigo:
    Hap-py birth-day to you (silabi 6 lkn YOU ni ndefu = mapigo mawili > 7)
    Heri ya ku zaliwa (silabi 7)
    Pole huku niliko ni asubuhi saa hizi. Kwa hivyo, hii ni kwa mwaka kesho sasa.

    Fri Mar 22, 05:31:00 pm 2013

    ReplyDelete
  24. Eh bwana Mama Jana kanivunja mbavu na wimbo wake wa kiswahili wa hepi basidei, nadhani tuupitishe uwe rasmi.
    Kweli jamii zetu hatuna utamaduni wa kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa ndio maana hatuna wimbo huu which is ok.
    Labda mtoto aelezwe ilo ajue harafu apewe wimbo wa Mama Jana maana tune yake inaeleweka ili hasiwe mpweke.

    ReplyDelete
  25. Mdau hapo juu unayeongelea mwarabu hatupi mila yake yani umekosea kabisa.... hakuna mwarabu hata moja aliye zaliwa na kuishi bongo anaongea kiarabu.... wote hawajui lugha yao sijui warabu gani unawaongelea.... ungesema wahindi ningekuelewa.

    ReplyDelete
  26. ukiona hivi ni wazi haya mambo sio yetu sisi tunaiga

    na hayana mpango wowote ule kwani wazee wetu waliotuzaa wakiyafanya haya na kulikuwa na hitilafu gani wakizikosa kwao hakuna sasa sisi tunaoiga ndio tunapasua kichwa kwa mambo ya kijinga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...