Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizunguma na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kabla ya kufungua mkutano wa siku mbili wa baraza hilo unaofanyika katika Hoteli ya St. Gasper mjini Dodoma. Wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edson Nyinyimbe. Kulia ni Katibu wa Tughe Mkoa wa Dar es Salaam, Gaudensia Kadyango, anayefuata ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Kaumo. Katika kikao hicho Dk Nchimbi aliwataka wafanyakazi waashirikiane ili kuleta mafanikio ndani ya wizara hiyo muhimu katika maendeleo ya nchi.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya kufungua mkutano wa wafanyakazi wa siku mbili unaofanyika katika Hoteli ya St. Gasper mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Felix Mwagara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Safi sana Dr Nchimbi kumbe wewe ni jembe ulikuwa wapi siku zote hizo?
    Kazi yako inatupa matumaini sisi raia wa kaiwaida wa Nchi hii ya Tanganyika na Zanzibar au Tanzania ukipenda kuita hivyo.
    Tunakufagilia Mtoto wa kihehe R.I.P

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...