Ndugu zangu,
Siku hii ya Kimataifa ya Wanawake haifai ikapita bila kujadili masuala ya msingi yenye kumhusu mwananmke na mahusiano yetu; wanawake na wanaume hususan kwenye kusaidiana malezi ya watoto wetu.

Kwa mwananme, mara nyingi jukumu la kumlea mtoto anamwachia mwanamke, haya ni mapungufu. Haitoshi tu kwa mwanamme kuacha hela ya chakula na mboga nyumbani. Kuna kufuatilia maendeleo ya watoto, ikiwamo shule.

Nitoe mfano, jana nikiwa hapa Morogoro kamanda wangu mmoja amenipigia simu akiwa nyumbani Iringa kuniomba nimsaidie na kazi yake ya shule kuhusu historia. Ananitegemea pia kuwa ni msaada kwake kwa mambo ya shule. Hivyo, ikanibidi niwaombe radhi wenzangu kuwa nisingekuwa nao baada ya saa kumi na mbili jioni kwa vile nahitajika nirudi nilipofikia na kuanza kazi niliyopewa na mwanangu. Kumsaidia kufafanua masuala ya historia. 

Hoja yangu hapa, ni kuwa wanaume, pamoja na majukumu yetu mengi, tuna wajibu wa kutenga muda nyumbani walau wa kuwauliza watoto wetu juu ya maendeleo yao ya shule. Kuyaangalia madaftari yao pia.

Na hapa mwanamme uanze kwa kujiuliza; Ni lini mara ya mwisho umeliangalia daftari la mtoto wako? Au ni kazi uliyomwachia mkeo tu?

Happy International Women Day!


MAGGID MJENGWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kipenda rahaMarch 08, 2013

    Mie Ni jana kuamkia leo

    ReplyDelete
  2. Kama hufungui daftari la mtoto wako ni wewe, usizani ni wanaume wote. Wenzako tunafungua na kucheki maendeleo yao kila siku, labda kama uwe umesafiri. Hata ukisafiri bado utaongea na mtoto kwa simu na kumkumbusha kufanya homework vizuri. Janjaluka.

    ReplyDelete
  3. Umeongea kitu cha kweli kabisa mjengwa, kwa sababu baadhi ya wanaume hawana/na hawajajingea mazingira ya kuwa karibu na watoto hasa katika maswala haya ya malezi anachojua yeye ni kutoa hela tu na wengine pia wanajua kuzalisha tu matunzo hawayajui kabisa. so mama km huna akili ya kuchakarika basi maisha ya watoto yatadolola hasa kielimu. TUNAOMBA WANAUME WENYE TABIA HIZO MBADILIKE. ASANTE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...