
Mwanamuziki wa siku nyingi Kabeya Badu (pichani), ambaye alikuwa anaimba katika bendi za Wazee Sugu amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Tafia ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Marehemu alikuwa akisumbuliwa na figo ambazo zilishindwa kufanya kaiz.
Wakati wa uhai wake, Kabyea aliwahi kufanya kazi na bendi nyingi zikiwemo za Orchestra Fauvetter, Orchestra Safari Sound, Marquis, Intimate Rhumba, Tancut Almasi na Wazee Sugu
Mola ampumzishe Mahala pema Peponi - Amina
Taarifa hii ni kwa mujibu wa mwanamuziki, John Kitime.
Video chini ikimuonesha marehemu Kabeya Badu (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na Wazee Sugu ukumbi wa La Prima jijini Dar.
MZEE KABEYA BADU R.I.P
ReplyDelete/Madau Vumbi Dekula
Namkumbuka na wimbo wake ZIADA alipokuwa na OSS, Mungu amlaze mahala pema Kabeya Badu
ReplyDelete