Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd,Absalon Kibanda akipakiwa kwenye ndege ya Kampuni ya Flightlink tayari kwa safari ya kwenda nchini Afrika Kusini kwa Matibabu baada ya kuvamiwa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na kujeruhiwa vibaya,alipokuwa akirudi nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, akiwa ndani ya Ndege ya Flightlink.
Absalom Kibanda akiwa na mkewe ndani ya Ndege, Anjella
Semaya, tayari kuanza safari ya kuelekea nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu.
Baadhi ya waandishi na viongozi wa jukwaa la wahariri wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi kwa ajili ya kumjulia hali.
Absalom Kibanda akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kusafirishwa kwenda Afrika ya kusini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Nyie mnaopenda kupiga,kuua,kutesa.Mtapiga wangapi?Mtatesa wangapi,mtaua wangapi?

    Nakuombea upone haraka Bro,familia yako inakutegemea sana.

    Na hii ni Challenge kwenu wana habari,mnatakiwa kujipanga na kukemea hii tabia CHAFU vinginvevyo hamtafanya kazi kwa uhuru-mtakuwa waoga.Hawa siyo majambazi,ni mchezo ule ule wa siku zote.Ankal usibane comment yangu yaani nina hasira hapa nilipo.

    David V

    ReplyDelete
  2. pole sana ndugu mungu atakutegemeza

    ReplyDelete
  3. Kuna maswali mengi ya kujiuliza zaidi ya majibu. Kwanini haya ya yanatokea? Ila muda huu ni wakuomba mungu aweke baraka zake kwa ndugu yetu apone haraka na arudi kwenye hali kama kawaida ingawa inauma sana kwa vitendo hivi vya kinyama

    ReplyDelete
  4. Ukitaka ubaya, dai chako!!!

    ReplyDelete
  5. Pole sana Kibanda, mwenyezi Mungu atakuponya haraka urudi nyumbani. Na shemeji yetu Mungu akutie nguvu.

    ReplyDelete
  6. ugaidi hauna nafasi kwa tanganyika hapo na wala hakuhitajiki fbi?

    ReplyDelete
  7. tatizo la hapa Tz wakuu hawapendi kuambiwa ukweli ,,ifike mahali wakubali kukosolewa ,,kwani ukiwakosoa tu umejichimbia kaburi

    ReplyDelete
  8. Ugaidi ni kitu kibaya sana. Haya magaidi yaliyofanya hiki kitendo yakamatwe yapewe adhabu inayostahili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...