Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) limesema litaifungia Tanzania iwapo itabainika kuwa Serikali imekuwa ikiingilia shughuli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
FIFA imesema kumekuwa na shutuma kupitia taarifa mbalimbali za vyombo vya habari nchini kuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeonesha nia ya kuingilia uendeshaji wa TFF.
Kwa mujibu wa barua ya jana (Machi 10 mwaka huu) ya FIFA kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, vyombo vya habari vimemkariri Waziri (Dk. Fenella Mukangara) kuwa Serikali imeiagiza TFF kutumia Katiba ya mwaka 2006 katika uchaguzi wakati tayari imeshafanyiwa marekebisho.
“Pia imeelezwa kuwa TFF imetakiwa kufanya Mkutano Mkuu pamoja na ule wa uchaguzi kwa tarehe ambazo zimepangwa na Serikali. Vilevile imeelezwa kuwa Serikali inakusudia kuunda Kamati ya Muda iwapo TFF haitatekeleza maagizo yake,” imesema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valke.
FIFA imesema iwapo yaliyoripotiwa na vyombo vya habari yatathibitika kuwa kweli, maana yake huo ni uingiliaji wa wazi wa Serikali kwa shughuli za TFF.
“Tunapenda kuwakumbusha kuwa wanachama wote wa FIFA wanatakiwa kuendesha shughuli zao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu mwingine kama ilivyoelezwa katika ibara za 13 na 17 za Katiba ya FIFA.
“Hivyo kama maagizo hayo yanayodaiwa kutolewa na Serikali yatatekelezwa, suala hili litapelekwa katika mamlaka za juu za FIFA kwa hatua zaidi ikiwemo kuisimamisha Tanzania kama ambavyo inakuwa pale panapokuwa na uingiliaji wa Serikali,” imesema barua hiyo.
Barua hiyo ambayo nakala yake pia imetumwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imeelezea baadhi ya athari ambazo Tanzania itakumbana nazo endapo itasimamishwa ni timu za taifa pamoja na klabu kutoshiriki mechi za kimataifa kwa mujibu wa Ibara ya 14 ya Katiba ya FIFA.
Vilevile si TFF au wanachama wake na maofisa wengine watakaoweza kunufaika na programu za maendeleo, kozi au mafunzo yanayotolewa na FIFA na CAF.
“Madai ya uamuzi uliofanywa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni ya kusikitisha kutokana na ukweli kuwa FIFA ilishatangaza itatuma ujumbe wake kuchunguza jinsi hali ilivyo kwa sasa na kutoa mapendekezo yake. Kutokana na hali hii, ujumbe wa FIFA uliokuwa uje kuchunguza (suala la uchaguzi) itabidi usubiri kwa vile ni muhimu kushughulikia tatizo hili kwanza.
“Katika mazingira haya tunaomba ueleze msimamo huu wa FIFA kwa mamlaka zinazohusika (Serikali) na athari ambazo mpira wa miguu wa Tanzania utakumbana nazo. Tunakushuru na tunatarajia utatufahamisha kila hatua inayoendelea katika suala hili,” imesema barua hiyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Sisi tulishajifungia wenyewe miaka yote,hata FIFA wakitufungia haitakuwa na Imnpact kama nchi za Nigeria,Cameroon,Burkina Faso,n.k
ReplyDeleteMaaumuzi ya Waziri lazime yaheshimiwe,FIFA nao wasiingilie masuala ya serikali yetu(Ni maoni yangu).
TFF wanapewa hela na serikali kwa kulipia kocha wa Taifa stars.
ReplyDeletePia sheria za Tanzania zinataka baadhi ya mambo yao yapate idhini ya serikali na hii TFF ipo Tanzania na wanaolalamika ni watanzania.
Iweje serikali yao isitake kujua kama kweli haki imetendeka?
FIFA waache ukoloni wa kimichezo!!!
Uncle hebu tutafutie na uiweke hewani hiyo barua ya FIFA kwa TFF ili tuisome kwenye lugha yake halisi ya kiingereza nasi tuweze kuitafsiri wenyewe
ReplyDeleteMambo yalikuwa rahisi, ila kwa kuwa kuna watu waliachwa ktk kinyang'anyiro cha uchaguzi ndio wakaanza vurugu, ooh katiba, oooh Tenga hafai. Na mawaziri wasiojua mpira wakajiingiza kati kwa kuwashabikia walioachwa, matokeo yake ndio haya sasa vurugu. Si kila mtu lazima aongoze mpira bwana, haiwezekani mtu adai 'hata tukifungiwa na FIFA potelea mbali' hawa si watu wa mpira, shawako sahihi kwa kuwa wafuasi wao wamepigwa chini katika uchaguzi.
ReplyDeletehuyu Tenga kaishiwa cha kufanya, anajaribu kutumia mgongo wa FIFA kukidhi matakwa yake. Hivi ni katiba gani inayopishwa kiujanja bila kufuata sheria na taratibu za nchi? Sasa yeye Tenga alitaka asisemwe hata kama mambo yamefanywa kiujanjaujanja.
ReplyDeleteHii ni janja ya toto kutoka TFF. Serikali wacha tufungiwe. Nigeria walifungiwa na sasa soka lao limerudi. Serikali wajibisha hao. Mbona ppesa za kudhamini makocha toka serikalini hawazikatai. Tenga amaliza uongozi wake vibaya!:)
ReplyDelete"Janja yake panya,Paka Kwisagundua"..Huo ni ujanja wa Tenga kumtishia mtu mzima nyau teehteeh..eti Tanzania tufungiwe??Kuna mashindano ya kimataifa tulioisha qualify toka akina Ndolanga/Rage na huyu tenga kama sio upuuzi tu wa kula pesa..huyu Tenga aondoke kule NA AACHE TUFUNGIWE ILI TUJIPANGE KAMA NIGERIA WALIVYOFUNGIWA!!!WALIPOACHIWA TU WAKACHUKUA ACON iwe sie hata hilo hatuqualify!!! ...
ReplyDeleteFifa na Serikali ni ipi yenye mamlaka juu ya nchi hii inayoitwa Tanzania?
ReplyDeleteHaya basi wacheni fifa waje kututawala.
Hawa FIFA ndio freemason wenyewe, wanajifanya wananguvu zaidi ya serikali kiasi cha kuingilia mamlaka yake, pumbavu kabisa. Serikali isimamie msimamo wako (isiwe legelege), watufungie, tujinoe ndani kukuza kiwango, then watatufungulia tu. Watabana mwisho wataachia...
ReplyDeleteHiyo FIFA yenyewe ukifuatilia michakato yake ktk Uchaguzi na uendeshaji wake imejaa Rushwa!
ReplyDeleteHivi hamuamini kama Raisi wa FIFA mwenyewe anapatikana kwa njia za rushwa???
Hamuamini kama wao wenyewe Mabosi wa Fifa ndio walio asisi biashara ya rushwa michezoni???
Hivyo pia usitegemee kama Fifa itaunga mkono waendeshaji wa mpira kama TFF kwa nchi wanachama wasio kuwa walaji na wa mipango kama wao.
Nafikiri wakifunga itafaa zaidi maana watakapo fungua hili GENGE LA KARATA TATU (TFF) ya sasa litakuwa limetoweka, ama tutakuwa tumejipanga kupata safu mpya Bora ya Viongozi kuliko kuendelea kutwanga maji kwenye kinu!!!
kweli ni nini???watu wanataka vigezo vya 2006 ili wawe viongozi???!!!kwani kama umekosa kuchaguliwa si ukae pembeni kwani huna kazi nyingine za kufanya!!au huko TFF kuna mahela watu wanakimbilia?
ReplyDeleteHapa bwana kweli kabisa janja ya mtu mzima kutishiwa nyau. Wewe muda wako ulio isha funga vilago nenda uswahini kaishi na uache kutafuta na kuweka watu ambao bado watakupa maslahi ukiwa huko mtaani. Tuache tamaa za madaraka na kutafuta watu muwajuao nyie kwa maslahi yenu binafsi bila kujali maendeleo na maslahi ya wengi. Si uungwana kutumiana. Mnang'ang'ania nini hapo kama tayari mmeshatumikia na muda wenu kuisha? Kuwa mtu mzima na mwenye ubinadamu. Acha tamaaa.
ReplyDeletekinachowasumbua watu ni hela sa fifa ambazo haijulikani zina fanya kazi gani coz kila event ya timu ya taifa bakuli linatembea so tukifungiwa itakuwa vizuri coz hela zitakata na tutapata viongozi wenye mapenzi ya kweli na soka letu na sio mapenzi ya fedha za fifa.TFF mbona mkiwa mnapokea mshahara wa kocha hamsemi serikali inaingilia soka.
ReplyDeleteFIFA ni kama UMOJA WA MATAIFA (UN)inaposhugulikia nchi mwanachama wake katika BARAZA LA USALAMA LA USALAMA la UN.
ReplyDeleteKwa vile Tanzania ni nchi mwanachama wa FIFA na Tanzania ilitia wino kukubali sheria, taratibu n.k za uanachama wa FIFA, basi wizara ya michezo Tanzania na TFF ni budi kufuata taratibu, sheria na kanuni za FIFA zinasemaje kuhusu migogoro ya TFF na wizara husika (serikali ya Tanzania).
Mgogoro huu si wa Rais Tenga au TFF au Wizara bali ni kuwa Tanzania kama mwanachama wa FIFA utatuzi wa migogoro sheria tulizozikubali za FIFA zinasemaje?
Mdau
Makini
Waziri kaza buti , usisikilize mambo ya watu wenye njaa mtaani, hapo TFF ni kakisiwa fulani ka- matapeli,WATANZANIA wenzangu amkeni mpira wa bongo una siri kubwa sana, hakuna lolote tulilovuna kwa ujanja ujanja wa watu wachache waliopo hapo wanaolinda matumbo yao.Hivi kwa akili ndogo tu hamuoni ujanjaujanja huo wa watu walewale kutaka kurudi TFF , HIVI HAKUNA MAMBO MENGINE MTAANI KAMA KUSHONA SUTI NA MENGINEYO? sioni hata mtu wa mpira hapo , bali wapo wanaohitaji kuneemesha matumbo.Tusiogope kufungiwa , vema tufungiwe ili tujipange upya , hapo utawaona watu wa ukweli wenye nia ya kuendeleza soka la bongo, Awali WACHINA walijulikana kama The sick men of the East kwakuwa walikuwa hawajimudu asilani kwa michezo, walijipanga wakaja kuwa wazuri sana kwenye Volleyball, Tutacheza michezo mingine soka ikiwa inajipanga na matapeli wakiwa wamefilisika.
ReplyDeleteTufike wakati mambo ya wananchi yaamuliwe zaidi na wananchi wenyewe badala ya Waziri au kiongozi tu.
ReplyDeleteSheria, kanuni na taratibu za FIFA na uanachama wake ziko wazi na hazihitaji serikali za nchi kuingilia mambo ya wanachama wao. Taratibu hizi ziliwekwa kwa ajili ya kuulinda mchezo huu ambao pia ni biashara kubwa sana duniani isitekwe na wanasiasa. Ni muhimu tujifunze hata nchi kubwa zilizoendelea vyama vyao vya mpira havifungamani na serikali kimaamuzi.
Ni jambo la kusikitisha kwaMh Waziri kuchulia suala TFF kana kwamba TFF ni chombo cha serikali, si kila chombo cha umma ni cha serikali. Kitendo cha Mh Waziri kimeonesha kwamba serikali inatumia mabavu zaidi hasa ukizingatia kwamba tayari Naibu wake alijitokeza hadharani kupinga maamuzi ya kukatwa kwa mmoja wa wagombea. Ni vema kukuza shughuli za kijamii hasa michezo, wizara ijikite kwenye kutengeneza na kusimamia sera zitakazokuza na kuleta maendeleo ya michezo jambo ambalo halifanyiki kwa ufanisi sasa hivi.
Ninamshauri Mh Waziri arejee mafaili ya mkasa kama huu ambapo serikali iliteua kamati ya Kanali Idd Kipingu ambapo maamuzi haya yalipeleka nchi kufungiwa hapa serikali ilipoamua kuiondoa kamati ya Kanali Kipingu, Mh Waziri ajiulize serikali inataka kurudia historia yake?
Hivi kote huku tumefika kwa sababu gani??? Malinzi kutolewa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi??? Ina maana asingekatwa kila kitu kingeenda sawa haya yote ya katiba imepitishwa kiujanja ujanja yasingesemwa. Sasa hapa tunapata picha gani? Kuna watu ambao ni lazima wawemo kwenye uchaguzi bila wao bora tufungiwe na FIFA??? Na mawaziri wasiojua mpira wanakuja na kauli za kujifanya wanatetea msimamo wa serikali kumbe wanamtetea Malinzi. Hypocricy of the highest degree. Ziliwahi kufungiwa nchi zilizotamba kwenye ulimwengu wa soka leo sisi tuna nini cha kuitisha FIFA??? Kama tuliamua wenyewe kuingia FIFA na masharti yao lazima tuyafuate vinginevyo basi tujitoe wenyewe kabla hatujafungiwa.
ReplyDeleteAcha Tufungufiwe kwanza,washike adabu,na tupate muda wa kujipanga upya!Timu gani za kwetu zinashiriki Africa Cup,au hata preliminaries za World Cup!Kwetu Simba na Yanga ndiyo kila kitu,tutafika kweli?Kuhusu uchaguzi wa TFF,katiba iseme wazi kwamba,wagombea wote waliopata kuwa viongozi waandamizi wa klabu za Simba na Yanga,au hata kati ya klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu,wasiruhusiwe kugombea katika uongozi wa TFF!sote tunajua madhara yake.wapo watanzania chungu nzima wenye elimu na uwezo wa kuongoza soka hapa nchini,nje ya viongozi au waliopata kushika uongozi katika Klabu za Simba na Yanga na nyinginezo!Kiburi cha baadhi ya "wanaofikiria kuwa kiongozi serikalini basi unaweza kuendesha mambo ya soka utakavyo"bila kufuata kanuni za FIFA,wajitayarishe,pindi Tanzania itakapo fungiwa na FIFA!msalaba wataubeba wao!
ReplyDeleteHawa wanalindana !
ReplyDeleteFIFA wanawalinda wala rushwa wenzao TFF wapo kama Genge la Mchezo wa Kamari ya Karata tatu:
Hebu angalia kwa uozo wa FIFA walishafikia kuchunguzwa na Shirika la Upelelezi la SFO (Serious Frauding Offences)!
Kwa taratibu zao, wameweka Mashirikisho ya nchi yasiingiliwe na Serikali ili kutoa mianya ya ulaji rushwa, mmeona sasa kwa nini Fifa inawakingia kifua watu kama TFF?
Sasa hapo tutategemea wao FIFA wawe wapenda haki?
Serikali iwaqeleze wazi Fifa ya kuwa kwa kuwa inatoa fedha za walipa Kodi kwa TFF Ruzuku kama ni lazima iingilie Shirikisho hilo!
ReplyDeleteKwa kuwa Serikali kupitia World Bank, UN na IMF ina uendeshaji unaoitwa PPP yaani (Piublic, Private Partnership).
Pia Fifa inahitaji ielezwe jinsi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyo ichukulia michezo ktk miale hii Mitano chini:
Zaidi ya Burudani Serikali inaitumia Michezo kama,
1.Kukuza ajira,
2.Kukuza Mahusiano ya Kidiplomasia na Kimataifa,
3.Kukuza muamako wa afya na uwezeshaji,
4.Kukuza Biashara na uwekezaji,
5.Kukuza ujenzi ktk Ustawi wa jamii na maendeleo yake.
Hivyo Serikali imewekeza kwa TFF kwa kutumia fedha za Umma ili kufikia azma 5 hizo hapo juu ambazo ni lazima ifuatilie kwa sababu hiyo.
Je, pana Ubia wa kibiashara anaoweza kuufanya mwekezaji bila kuwa na mazingira ya kushirikiana ipasavyo na uwazi???
Ni muhimu ili ijulikane kwa nini inaingilia masuala ya TFF, Serikali ifafanue mazingira hayo juu mbele ya FIFA!