Kuna mdau kaleta mzigo na special request ya ngoma hii ya 'Ikati' ya Condry Ziqubu. Asante mdau kwa kututoa machozi sie wa enzi hizo
Home
Unlabelled
ngoma azipendazo ankal
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
man oh maaaaan... hii kitu imenikumbusha mbaliii sana. Tuko secondary basi wkend lazima twende kuzisikiliza hizi nyimbo za sauzi.. very nice
ReplyDeletethx
I was six years! My brother played this when they were home for Christmas! It is amazing to recall back!
ReplyDeleteAsante Mdau! Hata majina yake sikumbuki ila nakumbuka midundo! I wonder if they still have the cassets now!
kibao hiki kinanikumbusha sembe na maharage yenye wadudu secondary. Tukimaliaza kupata msosi huo weekend wakati huo tumelikwa Rugambwa girls.Tunaenda kwa lori la shule na mwalimu wa nidhamu.Tulikuwa tukicheza tunzuiliwa kukaribiani na wasichana. Mziki ulipokuwa ukinoga mwalimu anatutenganisha kwa kiboko. Ahhh ama kweli Zakale ziondokile
ReplyDeleteAhsante Ankali kwa kuirusha Kete adimu angani!
ReplyDeleteSinger:Condry Ziqubu , Ikati song.
Mimi ndio niliomba Special Request, kwa kweli inabidi wengi tulie kama Wadau waliosema hapo juu.
Kwa kweli penye wengi hapaharibiki mambo, mimi nilitaja wiki iliyopita halafu Kiongozi Mkuu Mdau David V. wa humu Jamvini akanipa mwelekeo ni vipi goma hiyo nkuipata.
Ama kweli Mojmba wewe ni Msikivu kama Serikali ya Kikwete!
Duhhh Machozi machozi, machozi yananilenga lenga,!
ReplyDeleteKama tungeliweza kurudisha masiku nyuma kwa kweli pangekuwa patamu.
Ningejikuta nipo Disco nikiwa Kijana wa Sekondari mbichi miaka ya 1986-1988 nayaruka Madebe!!!
Ikitoka hiyo 'Ikati' DJ Ukimbini anaingiza wimbo 'Love Station' uliyoirusha wiki jana.
Ni bahati mbaya sana siku daima zinaenda mbele tu!!!
Wapinzani wetu sisi Za siku zile mpo wapi?
ReplyDeleteNinyi Watoto wa Kizazi Kipya wanyonge wetu mpo wapi?
Mpaka hapo Muziki huo tumesha wafunga Bao 3-0 na Mpira bado dk. 3 kwisha!!!
Hamtuwezi watu wazima sisi.
Hapo babake tupo ndani ya Disco pale Mbowe Hotels yaani Billicanas ya leo hii.
ReplyDeleteNi miaka ya 1986 hivi tunaruka hizo.
Ankali kwa kweli tutalia kwa mengi,kwa kuwa hizi zinapigwa tumepigika Kimaisha saaana,
ReplyDeleteBinaadamu sisi tunapita katika vipindi vingi sana vya kimaisha ,misukosuko, mabalaa, changamoto,Mitihani na Mafanikio, raha na tabu.
Na leo hii tunashukuru Mwenyezi angalau ametunusuru na Kutujaalia saana.
Mdau wa Lori la Shule Secondary School, anony wa Sat Mar 16, 08:44:00 am 2013
ReplyDeleteDuhh mlikuwa mnashikwa pabaya sana, Ukame wa Boarding School halafu Mziki ukinoga mnatenganishwa tena?
Ndio maana siku ya Graduation watu hufurahi sana kwa kuwa wanapindua Ukurasa wao wa maisha kutoka maisha ya Bweni 'gereza' kwenda kwenye maisha ya Uhuru!!!
Mojmba Michuzi ,
ReplyDeleteohhh wengi tunalia sana tukikumbuka miaka hii ya huu wimbo!!!
Ahhh jamani ni vile siku hazigandi!
ReplyDeleteWimbo huu nakumbuka nikiwa Sekondari Form 2 mwaka 1988,ulikuwa ukipigwa ktk msafara wa wasindikizaji Maharusi na nilipangwa kuwa Mcheza show ya wasindikizaji ktk Harusi.
ReplyDeleteSasa, unajua tena nafasi hizi zinakuwa ni adimu kwa vile wanatafutwa Wavulana(Ma-Handsome) wadogo wadogo na Wasichana(Ma-Beauty) wadogo wadogo tena wenye mvuto, basi ikatokea Broo mmoja (KIJEBA) sijui miaka ya uvulana wake hakupata kuchaguliwa kucheza?, ama ni ile huduma ya Daraja la kwanza wanayopewa kwa Kundi la wachezaji wa kusindikiza Harusi siku ya Sherehe ikifika , jamaa aka fosi Kingi akachaguliwa!!!
Ebwana eee, ile anaingia Kundini?, hata Mkufunzi wetu alipata kazi ya ziada kumwelekeza mpaka kwa taaabu ndio akaweza!
Alikuwa tukicheza wakati wa kugeuka, ohhh anageuka mzima mzima !!!, hadi Mkufunzi anarudia kumfundisha,
Kwa mushindwa kwake kugeuka wakati mziki huu ukipigwa wa Harusi tulimpachika jina na kumbita 'ASKARI WA KIHINDI' yaani kwenye Gwaride ikitoka amri ya kugeuka mziki huu ukipigwa yeye anageuka ndivyo sivyo!!!
Hahahahaha!!!
Watu sasa wanasema Laki si pesa!
ReplyDeleteLakini Muziki huo unapigwa Laki ilikuwa ni kama Bilioni na usheee hivi!
hawa south africa wana sauti ya asili ya kuimba ambayo mi naipenda sana lakini hawa masharobaro wetu wana kisauti flani cha kubana pua sijui kimetokea wapi!? yaaani hawaimbi free kama huyu anavyoimba - hapa the more unavyobana pua ndio the more una kipaji - sijui huu mtindo wa kubana pua utaisha lini ili watu waimbe free!
ReplyDeleteNakumbuka tulikuwa tunaimba kibwagizo chake "Nyerere Kamandoo" Dah! Ujamaa ulikuwa mzuri sana jamani.
ReplyDeleteMdau Houston (Yuston) TX
Ankal heshima yako mkuu.Naona una wapenzi wengi wa muziki wa "Bubblegum" kutoka Bondeni miaka hiyo.Si vibaya ukawatengea siku yao moja kwa wiki.Mimi nina Kabati limejaa Kanda/CD za muziki huu,ndo maana majina ya vibao na waimbaji havinipi shida sana.Vibao vingi bado vipo na vingi vinapatikana kwenye U-tube.Weekend njema
ReplyDeleteDavid V
Nyerere komando!
ReplyDeleteMzozaji
kweli kama anon mmoja alivyosema ingekuwa inawezekana kurudisha siku nyuma basi tungerudi kupata hizi raha tena.. Ila life goes on,
ReplyDeleteWe anon wa Sat Mar 16, 08:44:00 am 2013.. unasema ulikuwa unaenda Rugambwa girls ulikuwa shule gani? Mimi nilikuwa Ihungo tulienda saana Rugambwa, it was fun man.
Uncle next time tuwekee ngoma ya G-string ya Chicco.. safi sana
Anon wa Sat Mar 16, 11:00:00 am 2013.. unasema ukweli, south africa hawalembi lembi sauti. Wanatumia their natural voices na angalia vitu vyao vilivyokuwaga bomba kipindi hicho.
ReplyDeleteIla siku hizi sijui wameenda wapi, mbona hatusikii vitu vipya?
Nyerere Komandoo, Mungu akulindee
ReplyDelete