Ankal, wape vitu Ankal apendazo enzi hizo 'Mabrazameni' a.k.a masharabaro wa enzi hizo wakiwajibika kwa kwenda mbele na vitu vya uhakika iwe studio au live kama ktk clip hii kuanzia utanashati, mistari, uchangamfu, kutumia ala za muziki na kubwa zaidi kundi zima kufanya onyesho kama timu iliyokamilika idara zote na safu zote. Si wengine bali ni Kool & Gang live wakikupa 'Get down on it'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Uhhh ni raha muruwa kwa Mabrazameni a.k.a Vijana wa zamani!

    Staili kubwa ya uvaaji wa Kundi hili Kool and the Gang ilikuwa ni Maovaroli kila mmoja ktk wale 7 ya rangi tofauti tofauti.

    Kwa kweli Ma-Tozz wa Kitambo walikuwa wagumu, ni vile ukivaa overoli kwa sasa unaonakena ni Gangstar/ hardcore!

    ReplyDelete
  2. Masharobaro wa siku hizi, mmewaona Wakali wa Long time hao?

    Muziki wao huo mnauweza???

    Angalieni (sisi wa za zamani) walivyowafunika Ma-Tozz wa Kitambo,

    Masharo wa kisasa kazi kuvalia suruali makalioni, mmeona vijana wa kizamani hao walivyovaa pamba zao?

    Wengine mmepitiliza hadi mnavaa Bikini (Kufuli za Kike) zile zenye ukamba unaopita kati kutengenisha kalio moja na lingine!

    Hata kuimba wa sasa mna fosi mnabana pua zenu na kuimbia makooni, mmesikia sauti tamu inavyotoka na mmeona jinsi wanavyojituma Jukwani sambamba na kuvitumia Vyombo ki sawasawa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...