Hatimaye mnamo tarehe 09.03.2013, Watanzania tuishio hapa Nürnberg tulianzisha shirika(NGO) letu Pamoja e.V.
Dhumuni la NGO yetu ni: kuwaleta watanzania na wajerumani kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo kati yetu, mfano: huduma za jamii, kutangaza utamaduni kati ya Tanzania na ujerumani, kujifunza lugha ya kijerumani na kiswahili, kusaidia maendeleo ya nchi yetu Tanzania(huduma za mashuleni na mahospitalini), kushiriki na kuandaa hafla na matamasha tofauti hapa ujerumani.
Viongozi waliochaguliwa kuongoza Jahazi hili ni:
- Erick Morro (Mwenyekiti) na msaidizi wake Aneth Shubi Lwakatare
- Muzy Juma (Katibu) na masaidizi wake Rainer Thumm
- Rose Fett (Mwekahazina) na msaidizi wake Daniel Uphaus
Aluta Kontinua,
Erick M.
(Mwenyekiti, PAMOJA e.V- Nürnberg).
Mwenyekiti msaidizi akisisitiza jambo na katibu
akisikiliza kwa makini.
Washiriki na wanachama wakisikiliza kwa makini.
Mstari wa mbele aliyekaa chini wenye koti la
bluu ndio mwenyekiti Erick Morro. Mstari wa nyuma wa tatu kutoka kushoto mwenye
brause nyeusi ndio katibu Muzdat Juma. Mstari wa pili wa kwanza kutoka kulia ni
mwekahazina Rose Fett.
Ushirikiano wenu Wajerumani na Watanzania ni mzuri sana!
ReplyDeleteHao jamaa Wajerumani wanaaminika sana Duniani kwa jamii ya wachapa kazi, wakweli na wawazi ktk mambo...hio ndio mentality yao.
Hivyo tunategema mseto huo utazaa tija kubwa baina ya Jamii ya Ujerumani na Jamii ya Tanzania.
Safi sana !
ReplyDeleteMuwe mnapanga Ratiba ya ngoma za asili za makabila kwa kutumbuiza siku za wiki endi na mapunziko.
Mtakuwa mnaserebuka ngoma hizi,
1.Makindi ya Kizigua/TANGA
2.Mdumange ya Kisambaa/TANGA
3.Lizombe ya Kingoni/RUVUMA
4.Sindimba ya Kimakonde/MTWARA
5.Maswezi ya Kinyamwezi/TABORA
6.Behobeho ya Kikwere/PWANI
7.Mdundiko ya Kizaramo/DAR
Pia msisahau kuwavalisha Wajerumani Migolole na Rubega na Viatu vya makata mbuga wakati wa ngoma husika kulinga na Kabila.
Na pia mzingatie kuwa Taratibu za Mila na Jadi zinazingatiwa vilivyo huku ngoma ikitanguliwa na Dishi la asili la kulingana na Kabila ambalo ngoma inachezwa siku hivyo pamoja na utangulizi wa Tamthiliya na Hadithi za Kabila hilo.
Tudumishe Mila na Jadi !!!
Bigup watanzania wa ujerumani...ushauri wa Anon...namba 1 na 2 ni muhimu sana zingatieni. Nyie mnaonekama kwa sura tuu ni wasomi,vijana na wapiga kazi.
ReplyDeleteAsante.
SHIDA KWELI KWELI,JAMANI RUDINI NYUMBANI HUKU NI KAMA ULAYA TUU.
ReplyDeleteSafi sana hasa malengo yenu ya utalii na lugha ni mazuri sana. Fanyeni kazi kwa bidii sana kutimiza malengo, kusonga mbele na kupanuka zaidi.
ReplyDeleteUtamaduni, Mila na Jadi vinachangia maendeleo.
ReplyDeleteIsipokuwa ni zile Tamaduni, Mila na Jadi zisizokuwa potofu mfano kuwakataza watoto kula mayai, wanawake kula chakuala baada ya wanaume kumaliza kula na kusaza mamombo yao ndio wanawake wanakula, hii hapana kila kiumbe anastahili mlo wakiwemo wanyama wanaotuziunguka.
Tamaduni, Mila na Jadi zilizo na Tija ni mfano ile tabia ya Ushirikiano na Undugu ya jamii za Makabila yetu kwa miaka mingi, mfano Zile Mahakama zetu za Jadi zinazoitatua Migogoro na mfano Mabaraza ya Upatanishi wa Migogoro ya Wazee wenye Busara Kijijini, yakemkuwa vigezo vya mfano wa kuigwa hata kwa Tararibu za Mahakama za Kisasa (Modern Judicial systems).
Hivyo tudumishe Tamaduni, Mila na Jadi zenye tija!
Hahaha !
ReplyDeleteMliotoka Tanga baada ya ngoma za Makindi(Wazigua) na Mdumange(Wasambaa) muwakumbushe Wajerumani kuhusu Gazeti la TANGAMANO (Gazeti hili lilikuwa linachapwa kwa lugha za Kijerumani na Kiswahili Mjini Tanga wakati wa Utawala wa Mjerumani Tanga ilikuwa ndio Makao Makuu ya Serikali ya Mjerumani ,gazeti ambalo unaweza kuona Nakala zake ktk Vituo vya Makumbusho Ujerumani na Tanzania)
Mdau wa Pili anony wa Tue Mar 12, 02:50:00 pm 2013 Ngoma za asili umesahau KUBWA LAO,,,,KIDUKU (ya Waukaya/Wazaramo)!
ReplyDeleteKibwagizo chake:
Maneno kidogo Wazaramo haooo!
Maneno kidogo Waukaya haooo! X 3
Wajameni KIDUKU kipo sehemu zingine Afrika, hasa West Africa nilishuhudia;
-Mijini Lagos,Kano,Ibadan,Abuja na Kaduna , huko Nigeria ktk Viwanja Vikuu vya Mipira.
-Mjini Abidjan, Cote D'Ivoire ktk Uwanja Mkuu wa Mpira.
Nilishuhudia Mashabiki wa Timu
Uwanjani wakishabikia Timu zao huku wakipiga na kucheza Kiduku, wa nchi mbili tofauti nyakati tofauuti isipokuwa Nigeria walikuwa wanaimba kwa lugha za 'Makabila ya Ki-Hausa,Ki-Yoruba,Ki-Igbo na Ki-Ijaw' kulingana na eneo la mji na nilipofika huko Cote D'Ivoire walikuwa wanaimba kwa 'lugha ya Kreole' Jijini Abidjan.
Hivyo Kiduku ni zaidi cha Ki-AFRIKA !!!
Ebwana eeee msisahau ngoma ya Kimasai ile ya kupandisha Mori na Kuruka juu !
ReplyDeletePana Mdau alilalamika humu Jamvini ya kuwa kila mgeni akija nchini lazima afikr Arusha na lazima aonane na kukutana na jamii ya Wamasai, ni kuwa mambo kama haya ya Utamaduni, Mila na Jadi ndio yanawapa Pointi ndugu zetu Wamasai kuchaguliwa kutembelewa na wageni wengi zaidi kuliko sisi wengine.
Hivyo Ujerumani kwa Upende wa Tanzania nadhani Kundi lijumuishe Utamaduni na ngoma za Kimasai kwa kipaumbele pia na makabila hayo mengine ya nchini Tanzania.
Manawane kwa ngoma hizo hapo juu,
ReplyDeleteZa Madau wa Pili niwepo Mjini Nurenberg nikiwa On-Transit kuelekea Boston America nikiwa Hotelini kwangu nisikie sauti ya ngoma ya Makindi na Mdumange mimi Mgosi wa Kaya?,,,
Ahhh hata kama nina Ticket ya Business Class 'Confirmed'ya KLM ama Siwssair anayopanda sana Ankali Michuzi safarini kwa nini nisi cancell? ili nicheze Makindi na Mdumange na wandugu Ujerumani?
Niotaomba wanifunge 'segere' kiunoni na mkia wa ng'ombe mkononi na filimbi mdomoni ili nicheze!
Potelea mbali kama ni safari najua baada ya ngoma nitaendelea!!!
Samahani jamaa yangu wote wabongo(Mdau wa Tue Mar 12, 06:11:00 pm 2013) mnaofananisha Bongo vs Ulaya na Marekani. NI USIKU NA MCHANA, Haiwezekani. Nimebahatika kufika huko. Mwenyewe naipenda bongo sana, lakini nadhani kitu cha muhimu ni kukubali kasolo zetu ndiyo tujirekibishe kwa maendeleo.(Kwanza natoa wazo msome habari zilizopita humu March 9 kuhusu vyuo vikuu 10 ulimwenguni.)
ReplyDeleteMie nakaa kijijini kwani Dar majengo yapo lakini hamna miundo mbinu, na kila mtu anaelewa mvua ikinyesha tu, panakuwaje. Uchafu nje' nje'. Vile vile, Tanesco wanaweza kuchukua umeme wao wakati wowote, ilo alina ubishi. Tutafute mataifa mengine ambayo tunaweza kujifafanisha nayo(Labda Asia maana huk sijafika na nawaona wako wengi huku Magharibi), (Ndiyo napenda kwamba tunataka kujifafanisha na ulimwengu wa kwanza), ukweli hutabaki kuwa kweli
Anonymous wa Tue. March 12, 06:11pm 2013 ameshauri hawa watz warudi nyumbani kwa sababu nyumbani ni kama ulaya. Sijawahi kusikia ulaya watu wanakufa kwa kuumwa nambu wala kutumia vyandarua,kupeleka wagonjwa India/South Africa, matokeo yao ya kidato cha nne kufanana na yetu, wala nchi za ulaya kuomba misaada Tanzania. Sasa mdau unposema nyumbani ni kama ulaya, unamaana gani????? Nakubali kabisa kuwa Tz ni nyumbani, ndiko nilikozaliwa, ninaipenda sana nchi yangu na sina tatizo la kurudi. Tatizo langu hapa ni statement yako ya "..nyumabini huku ni kama ulaya tuu.."
ReplyDeleteMusisahau ugobogobo ngoma ya wasukuma toka mwanza. Lazima mucheze na nyoka futi nane. Nitumieni tiketi niwaletee.
ReplyDeletemsisahau ngoma ya kisukuma ya kucheza na nyoka.
ReplyDeleteMdau wa Wed 13, 05:33:00 am 2013 na Mdau wa Wed Mar 13,05:35:00 am 2013
ReplyDeleteNgoma ya Ugobo gobo kucheza na nyoka!
Itakuwa ni burudani maridadi sana na changamoto nzuri sana, itafaa wewe Mkufunzi uendeshe Darasa la Kisaikolojia kuwafanya wana Kikundi hasa Wajerumani wawazoee nyoka viumbe wanotisha kabla ya kuiweza kucheza ngoma yenyewe!!!