Sehemu ya pili ya WanaDMV wafanya mjadala wa kushuka kwa kiwango cha Elimu na matokeoa mabaya ya kidato cha Nne wakianza kuelezea Elimu zamani ilivyokuwa na nini kimesababbisha kuporomoka kwa Elimu Je nani alaumiwe na nini kifanyike kuokoa janga hili WASIKILIZE
Home
Unlabelled
MJADALA UGHAIBUNI, ELIMU TANZANIA SEHEMU YA PILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wakulaumiwa wa kwanza ni ninyi Madiaspora mliop Majuu ambao wengi wenu mlifika huko kwa masomo ya juu ikiwemo Fani ya Elimu.
ReplyDeleteCha ajabu ni kuwa baada ya kuhitimu Masomo yenu mkaendelea kubaki huko Ughaibuni badala ya kurudi nyumbani Tanzania kuja kufanya kazi ya Ualimu na kuamsha kiwango cha Elimu.
Hivyo ninyi mnaotoa mada wana DMV na Madiaspora wengine nchi zingine hasa mlio ktk taaluma ya Elimu, au Ukufunzi ndio wamojawapo wa kulaumiwa kuhusu kushuka Elimu nchini!
Lawama hizo ziwafikie licha ya kuwa pana mapungufu makubwa hapa nchini hasa juu ya Stahili na mafao ya wanataaluma wa Kielimu nchini, yaani maslahi madogo kwa waut kama Waalimu.
Licha ya kuwa unakta Wanasiasa (Mfano Wabunge) wanalipwa zaidi kuliko Walimu na Madakitari, kitu ambacho tunaqweza simama pamoja mambo yakarekebishwa.
Je, mliitendea haki Serikali na nchi yenu kwa kuaga kwenda kusoma na msirejee tena nchini?
Mawazo yangu ni haya:
ReplyDeleteUlaya unatumika mfumo huu na ndio maana kuna kiwango cha elimu.
1.Syllabus inatolewa kwa wanafunzi wote kabla ya mwaka wa masomo na haibadiliki miaka yote ni ile ile
2.Kunakuwa na learning outcome ya kila somo inayokuwambia masaa mangapi usome kila chapter NA unaambiwa maswali ya mtihani yatakuja katika topic hii au hii.
3.Kunakuwa na speciment question ambazo ukizipitia hizo mara kwa mara zinakupa general knowlege na rahisi kujibu maswali ya mtihani mfano kama trial tunaita TZ.
4.Kunakuwa na past papers and answers ambazo zinakuwa accessible kwa wanafunzi wote wakiwa wanazipitia mara kwa mara basi kupasi ni assilimia 70.
5.Kunakua na link na advice ya material ya masomo na wapi zinapatikana mfano library
6.Maswali hayaji nje ya zile learning outcomes
7.Masomo yanayosomeshwa yanaendana mfano ukisomeshwa biashara basi yanafanana labda customer service NA sio mara hku Geographia huku Sanaa inakuwa mwanafunzi amefeli form four hatoki na ujuzi.
haya ni kwa ufuppi tu nafikiri kiwango chety kitainuka sana na ongezeko la kupasi litakuwa juu na sio kukomoana unamsomesha mwanafunzi chengine na unamtolea swali jengine.
Maelezo mazuri kabisa. Je mtandao wa internet ambao kila kukicha unatangazwa kuwa umesambaa nchi nzima hauwezi kutumika kuendeleza elimu.
ReplyDeleteVijimambo mmenikuna sana na vipindi hivi vizuri. Ushauri wangu pelekeni kopi ya mijadala kma hii kwa wahusika kama serikali. Wakifanyia kazi wafanyie wakidharau mtakuwa mmetimiza adhima njema.
ReplyDeletegreat dialogue. good job Mube and all, bwana Matinyi na Rev. Shideko you nailed it, it was the funny truth lol....however, sidhani kama watanzania itawaingia. they still stuck in their own way of doing things. wanahitaji kuona umuhimu wa "know-how", and they need to be willing to change...on their own. ulimwengu wa sasa hivi siyo wa kufaulu mtihani only, rather wa kuweza kutumia knowledge waliyojifunza. and that speech ya naibu waziri wa elimu...it was a NO NO, a big NO kha!
ReplyDeleteall in all, this is the challenge
Anon wa 02:12, Ughaibuni kuna kazi za kumwaga kila sehemu wanahitaji wafanyakazi hata wewe ndio maana umebaki huko. TZ hakuna kazi kwa kila mtu, ndio maana mitihani ni kukomoana. Ikiwa kila mtu atapata First Class nani atapiga jembe. Ugahibuni mbeba box anapata mshahara sawa na karani au mwalimu.
ReplyDeletehii ndio barua niliyotuma kwa kamati iliyoteuliwa kufuatilia maswala ya kidato cha nne na upungufu wa elimu Tanzania.
ReplyDeletehttp://leadergennis.blogspot.com/
Madau wa kwanza hapo juu umenichekesha yaani meno yote tehelathini na nje mbili. Naomba tu mdogo wangu ufahamu kuwa ualimu ni taaluma. Si kila aliyesomea ughaibuni ni mwalimu. Tunapoamua kubaki mamtoni, tunawasaidia ninyi wadogo zetu mpate ajira ambazo otherwise tungepewa sisi endapo tungerudi. Kwahiyo kukaa kwetu huku, ndiyo mafanikio yenu kikazi. Huwezi kupanda bangi halafu unapovuna bangi unaunda tume ya kuchunguza eti kwa nini hujavuna mchicha. Mwalimu Tanzania anaonekana kama takataka halafu unata watu watoke mamtoni warudi kufundisha. Serikali inatakiwa itulie, ijali maslahi ya walimu, isafishe wizara ya elimu, wazazi wafanye kazi yao, watoto wapunguze fiesta na bata. Utaona baada ya miaka 5 kila mtoto atapata first class.
ReplyDeleteRushwa kweli ni adui wa haki. Watoto wa walala hoi hawapati elimu kwa sababu kuna mwalimu aliyehonga akapata cheti cha kufundishia, watoto wa vigogo wanasoma shule tofauti na za walala hoi na serikali inawajali zaidi wanasiasa kuliko walimu.Kuondoa ili tatizo ni kufuta wizara yote ya elimu na kuajiri upya kuanzia waziri na walimu na taasisi zote zinazohusina na wizara hiyo.
ReplyDelete