Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na makampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania.Airtel,Tigo,TTCL kuweka saini makubaliano ya pamoja ya kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma.
Baadhi ya wawakilishi wa kampuni za simu za mkononi wakimpigia makofi ,Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,mara baada ya kumaliza kutoa spichi yake wakati wa kuweka saini makampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania,Airtel,Tigo,TTCL kuhusiana na makubaliano ya pamoja ya kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma.
Mwakilishi wa Vodacom Tanzania Bw.Nguvu Kamando, (Kulia), akiweka saini makubaliano ya pamoja ya kampuni nne za simu za mkononi, kushiriki mfuko wa mawasiliano ya umma jijini Dar es Salaam . Katika mkataba huo makampuni ya Tigo, TTCL, Airtel ambapo Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Mnyaa,(Watatu kulia waliosimama), alishuhudia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Kamugisha Kazaura (Kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, Nguvu Kamando mara baada ya hafla ya kusaini mkataba wa ushiriki wa mfuko wa mawasiliano ya umma, jijini Dar es Salaam, ambapo makampuni manne ya simu za mkononi yameshiriki. Makampuni hayo ni Vodacom Tanzania, Tigo, TTCL na Airtel .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Huu mfuko wa mawasiliano ya umma lengo lake ni nini? Naomba nieleweshwe kwa kiswahili fasaha miye mswahili tafadhalini.

    ReplyDelete
  2. Mfuko wa Mawasiliano kwa wote una lengo la kupeleka mawasiliano katika maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara ili watanzania wote wapate huduma ya mawasiliano. Ili kufanya hivyo mfuko unashirikiana na watoa huduma za mawasiliano kwa kuwapa ruzuku ili kuwavutia kupeleka mawasiliano sehemu ambazo kibiashara wasingepeleka

    ReplyDelete
  3. Majina ya Mabosi hawa wawili matamu sana!

    1.Kamugisha Kazaura,
    2.Nguvu Kamando,

    Nakumbuka ktk Riwaya za Fasihi ya Kiingereza pana Kitabu kimoja kilitafsiri baadhi ya majina ya Kizungu kwa maana ya baadhi ya makabila ya Kiafrika na kukuta baadhi ya majina yakizungu yakimaanisha Kama:

    -(WAPE MBOGA NYINGI ZA MAJANI)
    -(MAAFA)
    -(HAPANA)

    n.k

    Lakini majina ya mabosi hawa wawili, ni Truly African, Real African!

    ReplyDelete
  4. Anonymous wa pili ahsante kwa ufafanuzi; nimeelimika vyema. Muumba akulipe haki yako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...