Weruweru river lodge hotel ya mjini Moshi imebainika kutumia umeme wa wizi mchana huu. Kikosi toka Tanesco makao makuu pamoja na mafundi mkoa Kilimanjaro wamebaini hotel hiyo kutumia umeme usiopitia kwenye mita. 
Mhandisi Francis Maze amesema hotel hiyo inamatumizi makubwa sana hivyo ni wazi kwamba Shirika limekuwa likipoteza mapato makubwa sana kupitia wateja hao. Meneja mkuu wa hotel na fundi mkuu wamechukulia na polisi kwa taratibu za kisheria.
Weruweru river lodge hotel ya mjini Moshi

Hivi ndiyo njia iliyowezesha Weruweru river lodge hotel kutumia umeme bila kupitia kwenye mita.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Audhubillah
    Naona wizi kama huu ndio unaoipa Tenesco matatizi, au niseme ndio inayoongeza matatizo ya Tenesco. Nionavyo mimi watu kama hawa wanyongwe. maana ni wizi wao unaotufanya tusiweze kutoka katika umasikini wetu.

    ReplyDelete
  2. Mangi wa KiboshoMarch 08, 2013

    Wanashirikiana na watu wa TANESCO hapa mjini Moshi mjue hilo!

    ReplyDelete
  3. Ninavyoelewa mimi ni kwamba hotel ni lazima zipate kila mwaka cheti cha safety and fire regulations. Sasa hotel hii iliwezaje kupata kibali cha kufanya biashara kama hiyo picha inavyoonyesha jinsi umeme ulivyokuwa umekonect. Kisha ikiwa wizi huu ulikuwa waendelea kwa muda, hao maakauntant wa Tenesco hawakuona kwamba bill za umeme ya hoteli hiyo ni chini kuliko inavyotarajiwa?
    Kuna mtu au watu waliokuwa wanakula nao kutoka kwenye sahani moja ya wizi.

    ReplyDelete
  4. masikini naamini angezolea mahabusu ila kwa mungu tutapata haki zetu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...