
Mkutano huo ambao kabla ya kufanyika kwake ulikuwa umepigwa marufuku na uongozi wa Simba kwa madai kwamba haukuwa halali ulifanyika kwenye Hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 600.
Mbali ya kumtimua Rage,mkutano huo pia ulimpendekeza aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans Pope na Rahma AL kharoos kuongoza kamati maalumu hadi pale uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakapofanyika.
Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Mohamed Wandi na katibu wake Maulid Said ulikuwa na agenda kuu moja iliyojadili mwendendo mbovu wa klabu ya Simba kwenye Ligi Kuu inayoendelea na kutokuwa na imani viongozi.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliokuwa na utulivu mkubwa huku ukilindwa na askari polisi wachache,Wandi alimlaumu Rage kwa madai kwamba amekuwa akiiendesha klabu yao pasipo kufuata katiba.
"Ibara ya 16 kipengele G inasema kutakuwa na mkutano kila baada ya miezi minne kujadili maendeleo ya klabu lakini haujafanyika mpaka leo.
"Vilevile ibara ya 18 kipengele cha sita inasema kamati ya utendaji itaunda baraza la wazee na kifungu cha 28 C,kutakuwa na nafasi ya mwanamke katika kamati ya utendaji lakini imekiukwa,huku ni kusigina katiba,".alisema Wandi na kuongeza kuwa:
"Ibara ya 22 ya katiba ya klabu ya Simba itupanawapata wanachama haki ya kuitisha mkutano endapo mwenyekiti na makamu mwenyekiti hawatakuwapo na ibara ya 19 kifungu cha tatu inatupa mamlaka ya kumwandikisha na kumfukuza mwanachama,".
Baada ya kumaliza kusoma sehemu ya katiba ya klabu ya Simba aliyodai imekiukwa,Wandi aliwataka wanachama wenzake kuamua kama Rage na kamati yake ya utendaji ipewe muda zaidi au iondolewe ndipo wot waliponyoosha mikono juu wakitaka watimuliwe.
Juhudi za Mwananchi kuwasaka viongozi wa Simba akiwemo Katibu Mkuu Evodius Mtawala na Msemaji wake Ezekiel Kamwaga ziligonga mwamba huku simu zao zikiiita pasipo kupokelewa.
Mwenyekiti wa mkutano huo, Mohammed Wandwi, akiongea na wanachama.
Wanachama wakinyoosha mikono kupinga uongozi uliopo madarakani.
Mwanachama Salum Simba, akiushutumu uongozi wa sasa.
Bi Hindu, mwanachama maarufu wa Simba, naye alitoa lake la moyoni kwenye mkutano huo.
Huyu Rage inaonekana ni ngumi mkononi....
ReplyDeleteHao walioitisha mkutano ni njaa tupu tusubiri wenye kujua sheria na pesa watakapo fikishana mahakamani maana sisi yanga ,yetu macho tu,na mkihitaji lori la fimbo lipo njiani.
ReplyDeleteNaona mnacheza tu ninyi hivi hamujui Mhe. Rage kuwa ni mtu makini sana.
ReplyDeleteSimb na Yanga a klabu nyingine maarufu wangefanya kitu kimoja. Waanzishe 'social clubs' na football' clubs'. Watu wanaopiga maneno tu bila kujua kinachotakiwa kwenye kuendesha mpira kisasa wabaki kwenye shughuli za ;zocial club' na mambo ya mpira yabaki kwenye mamlaka ya football club zinazoendeshwa kwa kanuni za uwajibikaji kama mashirika mengine.
ReplyDeleteWasiofaa waondolewe madarakani...si lage tu kuna makampuni mengi hapa daresallam yanaongozwa na wakurugenzi wasiofaa waliochaguliwa kwa njia ya uswahiba si ujuzi....
ReplyDeleteKuna kampuni moja ( jina tunalo) mfanyakazi wa kike ambaye hawezi kufanya mapenzi na mkurugenzi ananyanyaswa au kupelekwa sehemu asiyostahili...
Wakati mwingine akishaajiriwa huyo kahaba ndiye hutoa maamuzi ya kampuni kwa kumshauri mkurugenzi.
Serikali iliangalie hili haraka sana kabla hali haijawa mbaya...
Lakini huyo Rage mbona namsikia mwaka wa ishirini sasa! kila mara anatolewa na kurudi! hakuna jipya.
ReplyDeleteSasa mimi Rage mnaniambia nijiuzulu kwani ''NINACHEZA NAMBA NGAPI UWANJANI!''?
ReplyDeleteAkitoka India kwenye Matibabu na kukuta Mapinduzi yameshapita Msimbazi, ndio kwa mara ya kwanza ataitambua namba anayocheza Uwanjani!