Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya kusini mwishoni mwa ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini humo ambapo alihudhuria mkutano wa vyama vilivyokuwa mstari wa mbele katika harakati za ukombozi kusini mwa Afrika na pia aliongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC Troika jana.(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Wamependeza sana,Ingawa rafiki yangu Zuma kishikizo kimoja cha koti lake hajakifunga au kimefunguka.Kuna mdau humu amenifundisha kuchungulia sana hizi picha na kufanya observations,mwingine nimemwona hapo juu kwa CHIBIRITI ameshaona ile komputa za zamani.Blog ni burudani kweli kweli

    David V

    ReplyDelete
  2. Kaka kifungo cha chini cha koti hakifungwi...anaenda na wakati hivyo si kwamba kimefunguka au amekisahau lkn ndivyo ilivyo!!!

    ReplyDelete
  3. Acha ushamba wewe; si lazima kufunga kila kifungo cha koti la suti. Kufunga vifungo vyote kila wakati inachukuliwa kama kutokujua uvaaji suti. Suti zenye vifungo vitatu huwa vina majina yake:
    Kifungo cha juu huitwa Sometimes; kifungo cha kati huitwa Always; na kifungo cha chini huitwa Never.

    Maana yake sometimes kinafungwa; always kinafungwa na hakifungwi kamwe.

    Suti zenye vifungo viwili kile cha juu huitwa Always na cha chini Never.

    Suti ya kifungo kimoja huitwa Always.

    Jambo la msingi ni kwamba koti si kama shati.

    Acha ushamba.

    ReplyDelete
  4. Asante # 2 kwa kunielimisha.Kuelimisha ni kazi mojawapo ya BLOG,mimi kama binadamu siwezi kufahamu kila kitu.Sijasema Zuma kakosea,nimesema nimegundua kishikizo hakijafungwa.Mwalimu #3,ingawa umetumia lugha kali sana kunielimisha,lakini lazima nikushuru pia, nilikuwa sifahamu haya masuala ya NEVER,ALWAYS,haya mavazi ni ya Kimagharibi zaidi

    Mdau David V

    ReplyDelete
  5. In this wardrobe debate nitakubaliana na anon wa tatu. Kifungo cha tatu chini kwa kawaida hakifungwi. Ukiamua kukifunga ni sawa, ila wataaramu wanasema kisifungwe. Hivi vitu unaweza kusearch online kupata ideas

    my 2 cents

    ReplyDelete
  6. Usichingulie sana mavazi ya watu, hiyo ni sawa na kuweka pua yako ndani ya biashara za watu.

    Mbona hamjazungumzia lubega au msuli, kanzu nk. Maana navyo vinavaliwa na watu ktk blog hii. Makoti si yenu.

    ReplyDelete
  7. David msataarab sana!

    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...