Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Ukumbi huo umejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Xi Jinping wa China wakishangilia jambo wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wageni waliohudhuria sherehe za makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa China Mhe.Xi Jinping wakiangalia picha za matukio mbalimbali yanayohusu historia ya ushirikiano kati ya China na Tanzania katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo wakati wa sherehe za makabidhiano ya ukumbi huo jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa China Mhe.Xi Jinping pamoja na Mkewe katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere muda mfupi baada ya sherehe za ufunguzi wa ukumbi huo leo.picha na Freddy Maro,Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. wachina ndio wenzetu

    tunawahitaji sana wachina katika maendeleo ya taifa letu
    wachina wana msaada wa kikweli na wenye nia njema kiuchumi

    tanzania ni wakati mzuri wa kushtuka na mapema kujitenga na hawa wamarekani

    wamarekani ni marafiki wa masirahi

    tusisahau ule msemo wa marekani kuwa hawana marafiki wa kudumu isipokuwa wana masirahi ya kudumu

    wachina wanatusaidia kujenga nchi kupata vifaa vya gharama nafuu ukiangalia mpaka leo hii vitu vingi tanzania vilikuwa kama ndoto kuvipata na sasa vimejaa kila kona kutokana na mchina

    japokuwa shukurani ya punda ni mateke hatuchoki kuwabeza wachina kwa vitu vyao lakini ukweli utabaki palepale kuwa wachina wametukomboa kimaendeleo

    karibu sana mh xi Jinping

    ReplyDelete
  2. kaka michuzi mm mdogo lakini nataka kujua ni kitu gani muhimu ambacho waingereza walituachia katika utawala wao mpaka sasa ni faida kwetu mfano waejeruman reli ya kati wachina wamejenga reli ya tazar na majengo mazuri tz karibia yote ni wachina sasa hawa wa bibi nini ukubushwa wao na tujivunie asante sana nasubiri wadau

    ReplyDelete
  3. Waingereza wamepandikiza fitna; wagawe watawale ili waendelee kuchukua kiulaini kama Willium Sons Diamond, BG Group, n.k. Na mpaka tutakapotumia ubongo wetu ndiyo tutaleta maendeleo; yani SELF DETERMINATION. Tutafika tu kwa uwezo wa Muumba kwa kuwa dhulma haiwezi endelea milele.

    ReplyDelete
  4. Wametuachia muendelezo wa kujifunza historia za nchi za kigeni si ya Tanganyika. Tuliowengi hatujui katika ya mwaka 0 hadi 2013 TRANSITION ipoje? Wamejitahidi kutuharibia historia yetu na kutuletea feki; yani historia ya kwetu unaweza kuona inaanzia zaidi kuanzia 1884; hata hivyo nayo imechakachuliwa. Kwa kuwa tunaelezwa tu mkataba wa Berlin na vita vya maji maji; hakuna kingine. Yani hata hatujatajiwa shughuli za maendeleo tulizokuwa tunazifanya kabla ya hawa wazungu kuja. Je mwaka 700 kulikuwa na nini wakati kule ulaya wako gizani; hatujui. Na ukitafiti zaidi unaweza kuona kuwa tulikuwa tunatengeneza hela wenyewe na dola yetu ilikuwa imara sana huko nyuma; lakini hakuna anayejuwa haya yote. Lengo hasa ni kutufanya tuonekane hatujafanya kitu; yani CIVILIZATION imeletwa na wazungu na hapo ndipo wametuweka tuwe BRAIN WASHED na kila kukicha kujisikia hatuwezi n.k........

    ReplyDelete
  5. Wachina siku hizi warefuuu.....

    ReplyDelete
  6. Hivi hatuna majina mengine ya kuvipa vitu muhimu vya taifa. Kila kitu kninaitwa Julius Nyerere mwisho mpaka nchi itaitwa Julius Nyerere. Vitu tulivyoviita Julius Nyerere vinatosha jamani.

    ReplyDelete
  7. Wajerumani hawakutuachia reli bali ilibidi waiache,kwa sababu reli walijenga kwa ajili ya kusafirisha mkonge na meno ya tembo.
    Waingereza hawana cha kujisifia nini walituachia,labda sana sana walitusababishia madeni.
    Wachina nao si wabaya ..lakini tujiangalie maana sisi wafrika tunapenda sana kuwa tegemezi

    ReplyDelete
  8. waingereza wametuachia mfumo wa serikali za mitaa(counties, parish, mstahiki meya) wilaya, tarafa lakini sijui kwa vile tunachanganya mfumo wa serikali kuu kuhodhi kila kitu hata maamuzi ngazi ya halmashauri ndo maana tumekwama kila kitu lazima Ikulu na wizara mama iingilie.
    Mdau
    mfumo wa serikali za mitaa/wilaya

    ReplyDelete
  9. Badala ya kutoa maoni yanayolenga katika kutumia rasilimali zetu sisi wenyewe kuendelea, tunajadili nini CHA KUJIVUNIA tuliachiwa na wakoloni au kusaidiwa na China / Marekani. Yani elimu yetu haitusaidii hata katika kufikiri. Hii ni aibu wadau.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...