Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ufunguo kutoka kwa Rais Wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Xi Jinping wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Ukumbi huo umejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya China na Tanzania.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Xi Jinping wa China wakishangilia
jambo wakati wa makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wageni waliohudhuria sherehe za makabidhiano ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete na Rais wa China Mhe.Xi Jinping wakiangalia picha za
matukio mbalimbali yanayohusu historia ya ushirikiano kati ya China na
Tanzania katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere leo
wakati wa sherehe za makabidhiano ya ukumbi huo jijini Dar es Salaam
leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa China Mhe.Xi Jinping pamoja na Mkewe katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere muda mfupi baada ya sherehe za ufunguzi wa ukumbi huo leo.picha na Freddy Maro,Ikulu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa China Mhe.Xi Jinping pamoja na Mkewe katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere muda mfupi baada ya sherehe za ufunguzi wa ukumbi huo leo.picha na Freddy Maro,Ikulu.
wachina ndio wenzetu
ReplyDeletetunawahitaji sana wachina katika maendeleo ya taifa letu
wachina wana msaada wa kikweli na wenye nia njema kiuchumi
tanzania ni wakati mzuri wa kushtuka na mapema kujitenga na hawa wamarekani
wamarekani ni marafiki wa masirahi
tusisahau ule msemo wa marekani kuwa hawana marafiki wa kudumu isipokuwa wana masirahi ya kudumu
wachina wanatusaidia kujenga nchi kupata vifaa vya gharama nafuu ukiangalia mpaka leo hii vitu vingi tanzania vilikuwa kama ndoto kuvipata na sasa vimejaa kila kona kutokana na mchina
japokuwa shukurani ya punda ni mateke hatuchoki kuwabeza wachina kwa vitu vyao lakini ukweli utabaki palepale kuwa wachina wametukomboa kimaendeleo
karibu sana mh xi Jinping
kaka michuzi mm mdogo lakini nataka kujua ni kitu gani muhimu ambacho waingereza walituachia katika utawala wao mpaka sasa ni faida kwetu mfano waejeruman reli ya kati wachina wamejenga reli ya tazar na majengo mazuri tz karibia yote ni wachina sasa hawa wa bibi nini ukubushwa wao na tujivunie asante sana nasubiri wadau
ReplyDeleteWaingereza wamepandikiza fitna; wagawe watawale ili waendelee kuchukua kiulaini kama Willium Sons Diamond, BG Group, n.k. Na mpaka tutakapotumia ubongo wetu ndiyo tutaleta maendeleo; yani SELF DETERMINATION. Tutafika tu kwa uwezo wa Muumba kwa kuwa dhulma haiwezi endelea milele.
ReplyDeleteWametuachia muendelezo wa kujifunza historia za nchi za kigeni si ya Tanganyika. Tuliowengi hatujui katika ya mwaka 0 hadi 2013 TRANSITION ipoje? Wamejitahidi kutuharibia historia yetu na kutuletea feki; yani historia ya kwetu unaweza kuona inaanzia zaidi kuanzia 1884; hata hivyo nayo imechakachuliwa. Kwa kuwa tunaelezwa tu mkataba wa Berlin na vita vya maji maji; hakuna kingine. Yani hata hatujatajiwa shughuli za maendeleo tulizokuwa tunazifanya kabla ya hawa wazungu kuja. Je mwaka 700 kulikuwa na nini wakati kule ulaya wako gizani; hatujui. Na ukitafiti zaidi unaweza kuona kuwa tulikuwa tunatengeneza hela wenyewe na dola yetu ilikuwa imara sana huko nyuma; lakini hakuna anayejuwa haya yote. Lengo hasa ni kutufanya tuonekane hatujafanya kitu; yani CIVILIZATION imeletwa na wazungu na hapo ndipo wametuweka tuwe BRAIN WASHED na kila kukicha kujisikia hatuwezi n.k........
ReplyDeleteWachina siku hizi warefuuu.....
ReplyDeleteHivi hatuna majina mengine ya kuvipa vitu muhimu vya taifa. Kila kitu kninaitwa Julius Nyerere mwisho mpaka nchi itaitwa Julius Nyerere. Vitu tulivyoviita Julius Nyerere vinatosha jamani.
ReplyDeleteWajerumani hawakutuachia reli bali ilibidi waiache,kwa sababu reli walijenga kwa ajili ya kusafirisha mkonge na meno ya tembo.
ReplyDeleteWaingereza hawana cha kujisifia nini walituachia,labda sana sana walitusababishia madeni.
Wachina nao si wabaya ..lakini tujiangalie maana sisi wafrika tunapenda sana kuwa tegemezi
waingereza wametuachia mfumo wa serikali za mitaa(counties, parish, mstahiki meya) wilaya, tarafa lakini sijui kwa vile tunachanganya mfumo wa serikali kuu kuhodhi kila kitu hata maamuzi ngazi ya halmashauri ndo maana tumekwama kila kitu lazima Ikulu na wizara mama iingilie.
ReplyDeleteMdau
mfumo wa serikali za mitaa/wilaya
Badala ya kutoa maoni yanayolenga katika kutumia rasilimali zetu sisi wenyewe kuendelea, tunajadili nini CHA KUJIVUNIA tuliachiwa na wakoloni au kusaidiwa na China / Marekani. Yani elimu yetu haitusaidii hata katika kufikiri. Hii ni aibu wadau.
ReplyDelete