HATMA ya soka la Tanzania itajulikana kesho baada ya Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk Fenella Mukangara kukaa meza moja na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kujadili upya suala la uchaguzi wa shirikisho hilo.

Tenga aliomba kukutana upya na Waziri baada ya jopo la viongozi wa TFF wakiongozwa na katibu mkuu Angetile Osiah kufanya kikao na Waziri siku chache zilizopita  ambapo Waziri alitoa maagizo ya kuhakikisha hadi Mei 25 shirikisho hilo liwe limefanya uchaguzi wake na pia kuwataka waitishe mkutano wa marekebisho ya katiba kabla ya Aprili 15.

Kufuatia hali hiyo Tenga aliomba upya kikao na Waziri ili akutane naye mwenyewe ana kwa ana kwa kile alichokieleza kuwa serikali haipaswi kuingilia masuala ya TFF kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imeingilia uhuru wa TFF ambayo ni chama kamili kinyume cha matakwa ya FIFA ambapo kwa kufanya hivyo kutapelekea Tanzania kufungiwa.

Katika taarifa yake aliyoitoa wiki iliyopita Tenga alisema  “Suluhu itapatikana kwa mazungumzo kati ya Wizara na TFF. Naamini suala hili tutalimaliza baada ya kikao cha Machi 19 (leo) ambacho kimepangwa na Waziri kutokana na maombi ya TFF,” alisema  Tenga na kuongeza kuwa tatizo lilianzia kwenye mchakato wa uchaguzi ambao umesimamishwa na FIFA.

FIFA ilisimamisha Mkutano Mkuu wa uchaguzi baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa kulalamika, na yenyewe kuahidi kutuma ujumbe wa kushughulikia suala hilo hata hivyo ujumbe huo hauji tena hadi hapo TFF itakapomaliza na serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Fukuzeni huyo tenga na muweke Interim leader wa TFF. Wacha tufungiwe lakini Tenga asitengeneze mafia yake TFF. Hivi nani zaidi serikali au Tenga? Waziri usikubali kuyumbishwa, Tenga mtu mdogo tu hapa TZ.

    ReplyDelete
  2. Inaelekea cheo cha "rais" kinawapa kiburi TFF. FIFA haijawahi kusema kuwa chama cha mpira kisifuate taratibu za serikali ndio maana chama lazima kisajiliwe serikalini ndipo kitambulike FIFA. Hizi tafsiri za kuingiliwa zinatumiwa kwa kupindishwa makusudi kwa manufaa ya kundi fulani ambalo linaona TFF kama wengine hawastahili kuwepo!!

    ReplyDelete
  3. Inamana ujumbe uliotumwa kwenda kwa waziri na majibu yake Tenga hajauelewa ? Mimi naona ngoja tufungiwe ili tujipange vizuri mana hata hivyo tumechoka kuwa kichwa chamwendawazimu

    ReplyDelete
  4. nI BAADA YA KUONDOKA tENGA NDIPO TUTAKAPOUJUA UMUHIMU WAKE NA KWA NINI fifa na CAF wanamuamini.hizi kashfa anzopewa ni kutokana na demokrasia aliyoijenga ndani ya tff.sasa hebu awapishe hao wanaoitaka tff kwa hali na mali washike madaraka na kama kutakuwa na demokrasia tena kwani tutarudi enzi zile za kazi za tff kuendeshwa osini kwa mtu binafsi na sasa itakuwa cargo star

    ReplyDelete
  5. waliopata kuwa viongozi wakuu au waandamizi katika klabu kubwa za soka hapa nchini,hususan,simba na yanga,na sasa kuna azam,coastal,na nyinginezo,"wasiruhusiwe kugombea nafasi za juu za uongozi wa TFF,soka la Tanzania halitakwenda!huo ndio ukweli wenyewe!hatutaki TFF iwe na viongozi wenye ushabiki wa simba na yanga au azam na coastal!lazima wawe watu makini,wanaopenda soka,na hawakupata kuwa viongozi wa klabu za soka hapa nchini!kuondoa mgongano wa kimaslahi,period!FIFA wakitufungia,sawa tu,tupate muda wa kujipanga upya!Kwa maana hiyo,sioni kosa alilolifanya Tenga!Husda na unafiki tu wa baadhi ya mashabiki wa soka wenye mrengo fulani wa kiklabu!....soccer analyst.....

    ReplyDelete
  6. mdau wa pili umekosea sana, hujui kanuni na sheria za FIFA kabezo isa!!! Moja ya kanuni za FIFA ni kuwa vyama vyote vya michezo ya mpira wa miguu ni lazima viendeshwe kipekee (independently)bila ya kuingiliwa na serikali za nchi za vyama hivyo. Inaendelea kusema kuwa endapo serikali itaingilia na kujaribu kucontrol chama cha mpira kwa njia moja au nyengine, nchi hiyo itatolewa katika uanachama wa FIFA. Nchi nyingi zilijaribu huko nyuma zilijikuta zinafungiwa.
    Suali la vyama kujisajili katika nchi zao hilo ni suali jengine na ni sharti la nchi lakini haimanishi kuwa serikali ina uwezo wa kuingilia maamuzi ya chama cha mpira cha nchi yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...