Taasisi ya Maendeleo isiyo ya kiserikali ya Catherine Foundation ya jijini Arusha leo imetoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa wagonjwa Hospitali ya Mt Meru na vituo viwili vya Yatima vya Faraja na Lohada Moshono vyopte vya jijini humo.

Catherine Foundation Develeppent inaongozwa na Mbunge wa Viti Maalum UVCCM Arusha, Catherine Magigie.

Misaada hiyo ya vyakula na sabuni pamoja na kuwatembelea wagonjwa kufanyika ikiwa ni sehemu ya kuwapa faraja wagonjwa na yatima hao waki huu wa kuelekea siku kuu ya Pasaka ili nawao wajisikie ni miongoni mwa jamii.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida Mokit msaada wa mablang’eti ya kujifunikia wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mt. Meru ya jijini Arusha na kuwapa zawadi mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. inatia huruma sana kuwa sasa watu wanatumia shaida za watanzania kufanya biashara kama kila mtu akijitokeza basi tutaumaliza umaskini naona misaada yetu itazidi karibia na kampeni hazijaanza chadema hatukubali kudanganyika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...