Napenda
kuwafahamisha kuwa Mkoa wetu umepewa heshima na Wizara ya Maji kuwa Mwenyeji wa
maadhimisho ya 25 ya Wiki ya Maji Kitaifa yatakayo anza tarehe 16 Machi, 2013 na
kufika kilele tarehe 22 Machi, 2013.
1. Shukrani
Napenda
kuishukuru Wizara ya Maji kwa kutupa heshima ya kuwa wenyeji wa maadhimisho ya
Kitaifa ya 25 ya Wiki ya Maji.
Aidha,
navishukuru sana Vyombo vya Habari kwa kufika katika mkutano huu na kuwa tayari
kutangaza mafanikio yaliyowekwa katika Sekta ya Maji.
Naamini
maadhimisho haya yatakuwa chachu kwa wadau mbalimbali kuchangia kwa hali na
mali katika ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji Mkoani wa
Lindi.
2. Utangulizi;
Kila mwaka
kuanzia mwaka 1988, Tanzania imekuwa ikiadhimisha Wiki ya Maji kuanzia
tarehe 16-22 Machi kwa kuwahusisha wananchi na wadau wote wa maji.
Kilele cha
maadhimisho huwa ni tarehe 22 Machi ambayo siku hiyo inafahamika Kimataifa
kuwa ni Siku ya Maji Duniani kwa mujibu wa Azimio Na. 193/47 la Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa.
Uzinduzi
utafanyika tarehe 16 Machi 2013 katika Kijiji cha Mtandi Wilaya ya Kilwa na
Kilele cha Maadhimisho kitakuwa tarehe 22 Machi 2013 katika Manispaa ya Lindi
kwenye Uwanja wa Ilulu. Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho atakuwa
ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. JAKAYA MRISHO
KIKWETE.
Maadhimisho
ya Wiki ya Maji ya mwaka huu yataongozwa na Kauli Mbiu isemayo “MWAKA WA USHIRIKIANO WA MAJI KITAIFA”.
Madhumuni ya
Maadhimisho;
Madhumuni ya
Maadhimisho ya wiki ya maji ni pamoja na:-
·
Kuwaelimisha wananchi kuhusu Sera ya Maji na majukumu
yao katika kuitekeleza.
·
Kutathmini maendeleo ya Utekelezaji wa Programu
ya Maji, hali ya huduma ya maji na usafi wa mazingira na kuweka mikakati
ya kuboresha utoaji wa huduma na uhifadhi wa rasilimali za Maji.
·
Kuhamasisha wananchi na wadau wengine
kushiriki katika kupanga, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miradi ya
maji na usafi wa mazingira.
·
Kujenga mshikamano miongoni mwa wadau mbalimbali wa
Sekta ya Maji.
·
Kutoa ujumbe kwa wadau kuhusu Kauli Mbiu ya Wiki
ya Maji na Siku ya Maji Duniani.
Madhumuni
hayo yanalenga kuboresha utoaji wa huduma ya Maji, Usafi na
Uhifadhi wa Mazingira, pamoja na usimamizi na utunzaji wa rasilimali za Maji
nchini (vyanzo vya maji na miundombinu ya kufikisha huduma ya maji kwa
watumiaji).
3. Maandalizi
ya maadhimisho ya Wiki ya Maji mwaka 2013;
Maandalizi
ya Maadhimisho ya Wiki ya Maji yanaendelea vizuri na uzinduzi na kilele cha
maadhimisho kitawahusisha viongozi wa Kitaifa.
Maadhimisho
ya mwaka 2013 yanakusudia kuwashirikisha wananchi katika:-
·
kupanga, kujenga, kuendesha na kufanyia matengenezo
miradi ya maji na kuimarisha usafi wa mazingira,
·
kutunza vyanzo vya maji na kuwaelimisha wananchi juu
ya matumizi endelevu ya rasilimali za maji.
Matukio haya
yataenda sambamba na kutoa ujumbe (maudhui) wa Siku ya Maji Duniani ya
mwaka 2013 ambao ni “MWAKA WA
USHIRIKIANO WA MAJI KITAIFA”.
Shughuli
zitakazofanyika katika Wiki ya Maji hapa Mkoani Lindi ni pamoja na:-
·
Kuzindua miradi 3 ya Maji vijijini ambayo
ujenzi wake umekamilika.
Vijiji hivyo ni Mtandi (Wilaya ya Kilwa), Rondo Mnara
(Halmashauri ya Wilaya ya Lindi) na Luchelegwa (Wilaya ya Ruangwa).
Miradi hii imetekelezwa kupitia Programu ya Maendeleo
ya Sekta ya Maji na wadau mbalimbali.
·
Kuzindua
Mradi wa Uboreshaji Huduma ya Maji katika Mji wa Lindi kutoka chanzo kilichopo
katika eneo la Kijiji cha Sinde.
·
Kutakuwa
na Mikutano ya Hadhara maeneo yote ya Uzinduzi
Miradi yote itakayozinduliwa
itawanufaisha wananchi wapatao 134,108.
4. Kugharamia
Maadhimisho;
Ili kuweza
kugharamia maadhimisho ya Wiki ya Maji mwaka 2013, Wadau mbalimbali wameombwa
kutoa michango ya hali na mali ili kufanikisha maadhimisho haya.
Maadhimisho
ya kitaifa ya Wiki ya Maji yanagharimiwa na Wizara ya Maji , Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa, Mamlaka za Maji Safi na Maji taka nchini, Halmashauri, Taasisi na
Mashirika mbalimbali ya Kiserikali na yasiyo ya Kiserikali na Watumiaji Maji.
Napenda
kuchukua fursa hii kuwaomba wadau wote kutoa michango ya hali na mali ili
kuweza kufanikisha maadhimisho haya ya Wiki ya Maji Kitaifa yatakayofanyika
hapa Mkoani kwetu mwaka huu wa 2013.
5. Wito kwa Wananchi wa Lindi;
Nitoe wito
kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi kuwapokea na kuwakaribusha wageni wote ambao
watakafika Mkoani kwetu kwa nyakati mbalimbali katika Maadhimisho ya Wiki ya
Maji Duniani. Kipekee ninawaomba Wananchi/Wakazi wa Manispaa ya Lindi
kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
atakapowasili tarehe 21 Machi, 2013 na kuendelea kuwa nae mpaka siku ya Kilele
cha Maadhimisho katika Uwanja wa Ilulu tarehe 22 Machi, 2013.
Hiyo nyuma kwenye kalenda tunguli?
ReplyDeleteHapana. Ni cha kushikizia Pazia wakati likifunguliwa. Mzee Simbakalia yuu mbali sana na hicho ulichotaja! Ni Mcha Mungu.
ReplyDelete