Hotel ya kitalii ya Irente View and Cliff lodge yabambwa ikitumia umeme wa wizi mchana huu huko Lushoto,Mkoani Tanga. Hotel hii wameharibu mita kwa kuweka rezista kupunguza upimaji wa mita ili kujiwezesha kulipa kidogo sana. Hotel hii imekamatwa na kikosi maalum toka makao makuu ya Tanesco nchini kinachoongozwa na Meneja wa Huduma kwa Wateja wakubwa, Mhandisi Francis Maze. Mmiliki hajaweza kupatikana hivyo Tanesco wamekata umeme na kuondoka na mita na taratibu za kisheria zitafuata.Juu ni fundi kutoka Tanesco akikata umeme kwenye hotel hiyo.
Mhandisi Francis Maze wa pili toka kushoto, akimwelezea fundi wa hotel hiyo na maafisa wengine wa Tanesco kilichotokea.
Mita ya Irente View and Cliff lodge iliyoharibiwa kuruhusu wizi wa umeme.
Hivi ni kuwakatia tuu au kushtakiwa na kufungwa jela? Huu ni usanii sasa..
ReplyDelete