Kama Watanzania tuishio USA kwa pamoja tuko kwenye kushiriki diaspora world cup soccer kwa nia ya kufanikiwa kwenye medali za kimataifa, ili kuitangaza Tanzania katika miundo mbinu, utalii na vyote vinavopatikana nchini kwetu. 

Katika ushiriki wetu wa mwaka Jana tulianzisha timu na tulikuwa tunajulikana Kama Tanzania team tuliweza kushiriki kwenye Vijimambo Cup kama Tanzania DMV timu zilizoshiriki ni Malawi, Burundi, Atlanta Georgia, Star United na Tanzania DMV, tuliweza kuibuka washindi wa mashindano hayo na balozi wetu wa Tanzania nchini Marekani alitukabidhi kombe la ushindi, tembelea www.diasporaworldcup2013.com kwa matukio hayo.

Mwaka 2012 tulishiriki kwenye diaspora world cup na tukaweza kufika robo fainali na tuliweza kuzifunga timu kubwa kama Malawi, Spain, Cameroon na Ghana. Tumejifunza vitu vingi kwa mataifa mengine walivyo weza kuzitangaza nchi zao vikiwemo vyama vya michezo kutoka nchini kwao vilivosimamia katika uboreshaji wa nchi zao ili zifanye vizuri. Sisi kama waTanzania tunayo haki ya kupeperusha na kuitangaza nchi yetu kwa umoja na tukafanikiwa. Tunaomba Ushirikiano wenu.

Natanguliza shukurani zetu
Jabiri Jongo
Team Manager

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Duu,bendera ya TZ kichwa chini miguu juu!
    Kaazi kweli kweli

    ReplyDelete
  2. "bendera ya TZ kichwa chini miguu juu!
    Lazima iwe hivyo kwani hata Tanzania yenyewe wengi wao hapo hawajui vizuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...