Na Dixon Busagaga waglobu ya jamii,Moshi.
WADHAMINI wakuu wa mbio za Kilimanjaro Marathon, kampuni ya Bia ya
TBL, imekabidhi msaada wa magodoro na vyandarua kwa uongozi wa
hosptali ya Huruma na kituo cha Afya cha Uru Kiaseni kama sehemu ya
maandalizi ya mbio za Kilimanjaro marathon zinatarajia kufanyika machi
3.
Misaada ya aina hiyo hufanywa kila mwaka na TBL wakati wa maandalizi
a Mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo hufanyika kila mwaka ikiwa ni
utaratibu wa kampuni hiyo kurudisha faida iliyopatikana kwa wananchi
kutokana na utumiaji wa bidhaa zake.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Uhusiano na
Sheria wa TBL, Steve Kilindi, alisema kuwa TBL imeamua kufanya
utaratibu huo ambao wamekuwa wakifanya kila mwaka na mwaka huu
wameonelea ni vyema wakatoa msaada katika hospitali hizo.
Kilindi alisema kuwa msaada wa magodoro hayo 210 na vyandarua 200 ni
jitihada za kampuni hiyo kuhakikisa jamii ya Tanzania inafurahi na
kujivunia kilicho chao na kuongeza kuwa hicho wal;ichokitoa ni sehemu
ya shukuruni kwa watanzania ambao wamekuwa wakiwaunga mkono kila mara.
“Kama wadhamini wakuu wa mbio hizi, tumekuwa tukishiriki katika
shughuli nyingi za kijamii na moja yao ni kutoa msaada katika
mahospitali, leo tunatoa magodoro 210 na vyandarua 200 kwa hospitali
za Kiaseni ya Rau na Huruma ya Rombo, tunaamini katika hili tutakuwa
tuimesaidia kwa kiasi fulani,” alisema Kilindi.
Naye Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Ibrahimu Msengi akipokea
msaada huo kwa niaba ya uongozi wa hospitali hizo aliipongeza TBL kwa
kuamua kuijali jamii inayonunua na kutumia bidhaa zao na kuongeza kuwa
msaada huo anaamini utakuwa wa manufaa makubwa kwa wagonjwa katika
hospitali hizo.
“Moyo wa kutoa sio lazima uwe nacho, TBL wameonesha kuwa kazi yao sio
kutengeneza bia tu, bali wanaweza kujali jamii na katika hili
nawapongeza sana na ningependa mashirika na makampuni mengine nayo
yangekuwa yanafanya hivi,” alisema Msengi.
Msengi alitoa wito kwa wafanyabiashara wote na wamiliki wa makampuni
kuiga mfano mzuri ulioonesha na TBl na kusisitiza umuhimu wa kutoa
kwani jukumu la kuhudumia jamii ni la kila mtu na sio serikali pekee.
Kuhusu mbio za mwaka huu za Kilimanjaro marathon Dkt. Msengi alisema,
mbio hizo kufanyika katika ardhi ya Kilimanjaro ni fahari na kuongeza
kuwa matarajio ya wote ni kuona kila mtu akinufaika na mbio hizo huku
akiwatakia kila kheri wakimbiaji wote hasa wakimbiaji wa Tanzania.
“Nitumie Fursa hii kuwatakia kila la Kheri wakimbiaji wote wa
Kilimanjaro marathon, kila la kheri watanzania wote watakaotuwakilisha
keshokutwa naamini tutashinda,” alisema.
Kwa upande wake Mganga mnku wa mkoa wa Kilimanjaro (RMO), Dk. Mtumwa
Mwako, akipokea magodoro na vyandarua hivyo kutoka kwa kaimu mkuu wa
mkoa kwa niaba ya uongozi wa Hospitali za Kiaseni na Huruma, alisema
kuwa msaada huo utasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Malaria
kwa mama na mtoto.
Nao madaktari kutoka katika hospitali hizo, Dkt. Godwin Kiwelu wa
hospitali ya Huruma ya Rombo na Dk. Delfina Materu wa hospitali ya
Kiaseni ya Rau, walisema kwa msaada huo mzigo wa changamoto
zinazokabili hospitali hizo zimepungua huku wakisisitiza kuwa bado
kuna changamoto nyngi ambazo inatakiwa jamii inatakiwa kujitokeza
kusaidia kama walivyofanya TBL.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...