Na Ripota Wetu , Mwanza
Taasisi
ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imepongezwa kwa jitihada inazochukua
hivi sasa kuhakikisha kuwa sekta hiyo inakua imara, sauti moja na hivyo
kuchangia zaidi katika ujenzi wa uchumi.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti jijini Mwanza hivi karibuni Bi. Jovita Bubere na
Bw. Moses Nyaronga walisema TPSF imesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza
biashara zao na kuongeza mitaji.
“Tunaomba
taasisi hii iendelee na jitihada zake za kuwasaidia wanachama wake
mikoani ili kuendelea kutujenga katika kukuza biashara hasa kwa mikutano
kama hii ya kikanda kwa nchi nzima” alisema Mama Bubere wakati wa
mkutano ulioshirikisha wanachama wa TPSF kanda ya Ziwa.
Mama
Bubere ambae ni Mwenyekiti wa Asasi ya akina Mama Wajasiriamali
Tanzania, yenye makao yake makuu jijini Mwanza wanajishughulisha na
utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kama ususi, ushonaji na utengenezaji
wa vifaa vya majumbani.
“Tunahitaji msaada mkubwa ilikuweza kufikia malengo yetu,” alisema Mwenyekiti huyo. Akizungumzia
soko la Afrika Mashariki, Mwenyekiti huyo alisema wamejipanga vizuri
kuingia katika ushindani na tayari wameshaanza kutoa mafunzo kwa baadhi
ya akina mama kuhusiana na mbinu za kutumia ushindani unaokuja wa
kibiahsra.
Kwa
upande wake Moses Nyaronga ambae ni Mwenyekiti wa shirika la Lemon
Development Foundation lililopo katika wilaya ya Rolya Mkoani Mara,
alisema huu ndio wakati wa kuiunga mkono TPSF ili iweze kufanya kazi kwa
uhakika zaidi ya ilivyo sasa.
“Mikutano
ya namna hii ni mizuri, inatuleta pamoja kama wanachama na inasadia
kutoa mawazo kwa taasisi hii ili iweze kufanya vizuri zaidi,” alisema
Nyaronga. Akizungumzia
vijana kukimbilia ajira serikalini, Bw. Nyaronga alisema vijana wengi
wanatakiwa kujiunga katika sekta binafsi ambako kwa sasa ndiko kwenye
ajira nyingi hasa za kujiajiri.
“Sekta
binafsi imekuwa sana hapa nchini tofauti na miaka ya nyuma, nashauri
vijana wasitegemee ajira serikalini, waingie katika sekta binafsi,
kinachohitajika ni kuwezeshwa tu na hili linawezekana kama watajiunga
katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali” alisisitiza.
“Kuingia
katika magenge ya ajabu, kurubuniwa kwenda kwenye maandamano ni ukosefu
wa maarifa, na hii inachangiwa na vijana wengi kukosa mwongozo wa nini
wachague na nini waache na kwa wakati gani, wakielewa hilo
watabadilika,” alisema Nyaronga.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw. Geofrey Simbeye, alisema taasisi hiyo ina lengo la kuweka
mazingira bora na wezeshi kwa wanachama wake katika kuongeza kasi ya
uanzishwaji wa makampuni na viwanda kwa ajili ya kuongeza ajira na
kuinua uchumi wa nchi.
Alisema pia taasisi hiyo inataka kuishawishi serikali kuondoa baadhi ya vikwazo katika ufanyaji biashara ndani na nje ya nchi. Alisema
TPSF inataka wanachama wake wafahamiane katika ufanyaji biashara hasa
katika mikoa iliyopo katika kanda moja pia kujenga kongano (clusters)
imara zitakazoweza kuwaunganisha katika sekta mbalimbali za kiuchumi.
Mkutano
huo wa siku moja uliofanyika jijini Mwanza ulikuwa na lengo la
kuelimisha na kuhamasisha muundo wa uwakilishi katika kongano (clusters)
na kuhusisha mikoa ya Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza,
ambayo inaunganisha kanda ya ziwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...