Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akionyeshwa vifaa vya kufungia samaki kabla ya kusafirishwa nje ya nchi na meneja udhibiti ubora wa kiwanda cha samaki cha Vicfish mjini Mwanza Bw Jacob Maiseli.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akipata Maelezo ya Utengenezaji wa Samaki na Meneja udhibiti ubora wa kiwanda cha samaki cha Vicfish Bw Jacob Maiseli wakati wa Ziara ya kulembeleana kukagua Uchafuzi wa Mazingira JIjini Mwanza.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akitoa Maelekezo kwa Meneja Udhibiti Ubora Bw Jacob Maiseli kuhusu Mfumo wa Maji taka wa Kiwanda cha Samaki cha Vicfish cha Jijini Mwanza aliofanya Ziara ya kutembelea na KujioneaUchafuzi wa Mazingira.


Uelelwa mdogo kwa wananchi juu ya suala zima la uhifadhi na usimamazi wa mazingira, imeelezwa kuwa ni moja ya changamoto ya usimamiz wa mazingira katika jiji la mwanza. 

Hayo yameelezwa leo na Afisa Mazingira wa mkoa mwa Bw. Charles Amani wakati akiota taarifa kwa naibu wazir Ofisi ya Makamu wa Rais katika Ziara ya kutembelea viwanda mjini Mwanza.

Pamoja na changamoto hiyo mkoa pia unakabilina na upungufu wa vifaa vya udhibiti wa taka ngumu na kutokuwepo kwa teknolojia ya ufuatiliaji wa uchafuzi wa mazingira kwa hewa kutoka viwandani na kwenye magari pamoja na kutokuwa na dampo la kisasa.

Bw. Amani maeeleza kuwa pamoja na changamoto hizo, jiji la mwanza limekuwa likiongoza kwa usafi wa mazingira kwa kipindi cha miaka saba mfululizo, kutekelezaji wa kampeni ya upandaji miti pamoja na miradi mbali mbali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Charles Kitwanga ameeleza kuwa lengo la ziara yake mkoani Mwanza si kufungia viwanda bali ni kutaka kuwa na msimamo wa pamoja na kuzingatia na kutekeleza sheria ya usimamizi wa mazingira, ili iwe yenye manufaa kwa watanzania, “lengo la kuja ni kuhakikisha sheria inafuatwa” alisisitiza.

Mh. Waziri aliongeza kwa kusema kusema kuwa ni vyema Halmashauri na wizara husika zikajipanga ili kuona namna ya kuwapatia sehemu mbadala wananchi wanaoishi milimani bila kuwabugudhi, ili kule nako kupangwe ili kuwe na mazingira endelevu.

Wakati huohuo, kamanda wa police wa kikosi maalum cha mazingira Nchini Bw. George Mayunga ameeleza kuwa jeshi la police lipo tayari kupambana na wahalifu wa mazingira,ili kujenga mazingira endelevu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Si kweli wale waliotengeneza filamu kwamba Watanzania tunakula vichwa na mifupa ili hali minofu wanapelekewa wazungu! hiyo pcha inaonyesha ukweli kiasimtanzania wa kima cha chini hawezi kumnunua huyo samaki! au nasema uongo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...