Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 - Kuchomoza kwa Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai akisema kwa mujibu wa ripoti hii mwaka huu iaonekana kuwa Tanzania tumefanya vizuri na kiwango chetu kimeongezeka kama ngazi mbili ikilinganishwa na ripoti iliyopita.
Hata hivyo amesema kwa bado kuna mikoa mingi ambayo unapopima maendeleo kwa ujumla wake mikoa mingi ipo asilimia 20 hadi 30 ambapo hii inapima ujumla wa maendeleo katika Jamii.
Bw. Lyimo amesema kwa sasa serikali ina mipangp mizuri ya kuisaidia mikoa hiyo, akitolea mfano kilimo kuwa kuanzia miaka ya 80 hatukuiangalia vizuri tulikuwa na taasisi za kilimo, mashirika ya maendeleo ya viwanda lakini katika kipindi hiki cha mageuzi tumepata matokeo mazuri.
Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 ikiainisha Kuchomoza kwa Nchi za Kusini:Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai ambapo amesema sera kabambe, zilizotengenezwa vizuri zinaweza kufanya mafanikio ya kimaendeleo ya binadamu kuwa endelevu katika miongo ijayo na kupanuka kufikia nchi nyingi zaidi zinazoendela.
Lakini pia Dkt. Kacou ameonya hatua za kubana matumizi zisizo na mtazamo wa mbali, zaweza kushindwa kushughulikia hali ya kukosekana usawa, na kukosekana kwa ushiriki wa maana wa jamii na kutishia maendeleo haya kama viongozi hawatachukua hatua za kurekebisha.
Aidha amesema baadhi ya mataifa yanayoongoza kwenye nchi za Kusini yanajenga mwelekeo mpya wa kukuza maendeleo ya binadamu na kupunguza tofauti za kimaisha kwa kuweka sera bunifu ambazo zinasomwa na kuigwa sehemu nyingine duniani.
Baadhi ya Wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini wakimsikiliza Dkt. Alberic Kacou (hayupo pichani) alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 iliyofanyika jijini Dar leo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mnaona Ripoti hiyo?

    Tanzania imepaa Kimaendeleo!!!

    Kazi ya Mhe.Raisi Dr.Jakaya Mrisho Kiwkete ndio hiyo, mtake msitake Tanzania imeendelea na imepiga hatua.

    1.Angalieni Ripoti ya Worldbank kasi ya kukua kimaendeleo Tanzania mwaka huu 2013 itakuwa ni 6.4% kwa mwaka (Wastani huo ni juu ya wa Dunia ambao ni 5%), hawa jamaa Worldbank ni kama wale Waalimu wagumu kutoa Maksi Shuleni wakikupa ujue kweli umefumua Mtihani!!!

    http://www.worldbank.org/en/country/tanzania

    Tena ilikisiwa kuwa GDP Growth iwe 7.1% ni vile kumetabiriwa na kufikia hiyo (6.4%) kutokana na mtikisiko wa Kiuchumi kufuatiia Uchaguzi Mkuu wa Kenya, nchi iliyokuwa mhimili Kiuchumi ktk EAC.

    2.Jamhuri ya Kenya, inafanya mchakato wa kukopi Mpango wa Kilimo wa Tanzania kwa kuona mafanikio yake (Kama mnavyoona hapo kwenye Ripoti ya UNDP) ingawa Kenya imepiga hatua kwa Utafiti wa Kilimo kwa Mpango wa Miradi ya GMO ingawa inapingwa na wengi.

    Chama kimoja cha Upinzani (kwenye mabano) wenyewe mnakifahamu mtajaza watadai wanakataa ukweli huu!

    Hivi Shirika kama UNDP na Mashirika yanayohusiana nao wanaweza kutoa Ripoti ya Uongo?

    ReplyDelete
  2. Chadema Ripoti kama hizi mnafuatilia kweli?

    Ni wazi sasa kama CCM imeshafanya kazi kama hivi mnavyoona ktk Ripoti ya UNDP-2013 kilichobaki ninyi mkafanye kazi za Kujitolea za Kijamii kama kuzibua mifereji ya maji taka na Huduma za Jamii!

    Maana mtakosoa nini tena?

    ReplyDelete
  3. Kitu hicho kulaleeeki!

    Ripoti ya UNDP ya mwaka 2013,

    Hapa sasa Wapinzani ni Timu moja hapa nchini Tanzania wenyewe mnaifahamu na Serikali ya Chama cha Mapinduzi ni F.C Libolo !!!

    Hivyo hiyo timu (Wapinzani) inapokutana na Serikali ya Chama Tawala a.k.a (F.C Libolo) ndio pale unakuta watu wanaacha kazi wenyewe Klabuni, na mambo yanakuwa mshike mshike Klabuni!

    ReplyDelete
  4. Safari hii Chadema na Upinzani mtazaa na sisi Sisiemu!

    Inaonyesha mmeegemea sana kwenye Siasa za Jazba na kukurupuka huku mkiwa Ripoti kama hizi kamwe hmafuatilii kabisa.

    Licha ya Ripoti ya UNDP kutolewa kama hivi usije shangaa Kiongozi wa Chdm tena Msomi akaja na zake za kuleta, kama vile taarifa hii hajaisoma?

    ReplyDelete
  5. Vyama vya Upinzani mna mpya leo hapa Jamvini?

    Ninyi hasa kile Chama cha Kabila moja hivi mmekuwa kama mwanamke asiye ridhika, unaweza kumchapa na mtambo weee!!!, halafu akinyuka anabeba kufuli lake anasema bado naenda kwingine!

    Ohhh, nchi haija endelea, ohhh tupo nyuma!

    Taarifa ya UN hiyooo sijui mtasema nini?

    ReplyDelete
  6. Mtasema ohhh Ripoti ya UNDP ni ya CCM!

    Wajameni UNDP na CCM wapi na wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...